Udugu wa Kiislamu ni hatari kwa mshikamano Ufaransa
21 Mei 2025Vuguvugu la Udugu wa Kiislamu Muslim Brotherhood ni kitisho kwa mshikamano wa kitaifa nchini Ufaransa na hatua lazima ichukuliwe kuzuia kuenea kwa uislamu wa kisaisa.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti inayotarajiwa kuwasilishwa leo kwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Ripoti hiyo ambayo nakala yake ilipatikana na shirika la habari la Ufaransa AFP jana Jumanne inasema ukweli wa tishio hilo, hata kama ni la muda mrefu na halihusishi vitendo vya ukatili, unaleta hatari ya uharibifu wa muundo wa jamii na taasisi za jamhuri na kwa upana zaidi, kwa mshikamano wa kitaifa.
Macron awakaribisha viongozi wa Ulaya kuizungumzia Ukraine
Ripoti hiyo, iliyotayarishwa na watumishi wawili wakuu wa serikali, itachunguzwa na Baraza la Ulinzi la Ufaransa leo Jumatano. Ufaransa na Ujerumani ndizo zenye idadi kubwa ya Waislamu miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.