Udondozi wa magazeti ya Ujerumani leo
27 Juni 2005Magazeti niliyonayo hapa studioni ni General Anzeiger linalochapishwa hapa Bonn, Mittelbayerische Zeitung la kutoka Regenburg, Markische Oderzeitung kutoka Frankfurt, Kolnischer Zeitung, Stuttgarter Zeitung na Frankfurter Allgemeine.
Mada kuu iliyopewa kipao mbele na magazeti yote haya ni matokeo ya kushangaza ya uchaguzi wa urais uliofanyika nchini Iran. Gazeti la General Anzeiger limeutazama ushindi wa meya wa zamani wa mji wa Tehran, Mahmoud Ahmadinejad na wasiwasi. Gazeti linasema ushindi huo ni wa kuridhisha, kwani umeweza kutimiza lengo la kundi la kikosavativ, la kurejesha tena umoja wa kidini na kitaifa nchini Iran, baada ya juhudi za miaka minane.
Kuchaguliwa kwa Mahmud Ahmadinejad kuwa rais mpya wa Iran kuna maana kwamba taasisi zote za kitaifa zimo mikononi mwa maongozi ya kiislamu. Kuongezeka kwa upinzani dhidi ya mataifa ya magharibi na maongozi ya kiislamu yanayoyapinga maadili ya kiliberali, yataathiri siasa za nje, maendeleo nchini Irak na uhusiano na Marekani. Pia wapatanishi wa umoja wa Ulaya wanaotaka Iran ikomeshe mpango wake wa nuklia, tayari wanahisi juhudi zao zitaathirika.
Gazeti la Mittelbayerische kutoka mjini Regenburg laandika. Wizara ya ulinzi nchini Marekani, Pentagon, inatakiwa sasa kuongeza saa zake za kufanya kazi, kufuatia kuchaguliwa kwa Mahmoud Ahmadinejad, kama rais mpya wa Iran. Hii ni kwa sababu hata baada ya rais George W Bush kushawishika kwamba Iran ni maficho ya magaidi, amechaguliwa rais mwenye msimamo mkali wa kidini.
Meya huyo wa zamani, hajaiweka siri azma yake ya kutaka kuyaongezea nguvu maongozi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa nuklia. Hilo ni jambo linaloipa wasiwasi mkubwa serikali ya Washington, limeandika gazeti hilo. Kufuatia uvamizi wa Irak, ulioongozwa na Marekani, Iran imekuwa katika orodha ya rais Bush ya mataifa ambayo yanadhamini ugaidi.
Gazeti la Markische Oderzeitung kutoka mjini Frankfurt laandika. Ni kweli kwamba serikali ya Tehran inataka kutengeneza bomu la nuklia lakini hakuna ushahidi wowote. Russia na China zitategemewa wakati Iran itakapofikishwa mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa. Serikali ya Moscow na Peking zinaendeleza maslahi yao mengi nchini Iran na zinaweza kutumia kura yao ya turufu kuvipinga vikwazo vitakavyowekwa na baraza hilo dhidi ya Iran. Kwa mtazamo huu, njia ya pekee ya kuizuia Iran kuendelea mbele na mpango wake wa nuklia, ni uvamizi wa kijeshi, ambao Marekani bado hauj