Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo
30 Septemba 2004Gazeti la shughuli za biashara HANSDELSBLAT, kuhusu waraka ambao wanasiasa wa nchi za magharibi, wakiwemo wa vyama vya kisiasa vya Ujerumani vya Kijani na CDU, kwa rais wa Russia Wladimir Putin, linaandika: Putin ni mwenye kupitisha maamuzi peke yake, lakini si dikteta. Iliwabidi watiaji saini waraka huo kutambua hayo kwanza, kabla ya kumweleweka vingine rais wa Russia. Kwa kweli ni barabara na muhimu kukosoa hali ya maendeleo nchini Russia, lakini mtu asije atatilia chumvi sana, kama sivyo ukosoaji huo utaelewa kwa njia nyingine.
Kuhusu hali nchini Irak baaada ya wasaidizi wawiwili wa kike wa Italia kuachiliwa huru, gazeti la LÜBECKKER NACHRICHTEN linaandika. Inaweza kutumainiwa tu kwamba, kuachiliwa huru wanawake hao wawili wenye majina yanayofanana ya Simona, kutawafanya wanasiasa kurekebisha misimamo yao kuelekea Irak. Nayo ni kutambua kwamba, amani na demokrasia katika Irak, inaweza kuhifadhiwa tu, chini ya himaya ya umoja wa mataifa. Lakini kama hali ilivyo sasa, hii ni kama ndoto ya mchana. Labda hali hii itabadilika baada ya uchaguzi nchini Marekani.
Ijapokuwa serikali ya Italia inakanusha kwamba, wanawake hao wawili waliachiliwa baada ya kulipwa kiasi fulani cha pesa kilichodaiwa na watekajinyara, gazeti la mji wa Lüneburg LANDES-ZEITUNG, linasema: Waziri-mkuu wa Italia, Berlusconi, sasa analipa pesa kwa mafunzo ya wale wanaokosea katika imani, ambao wanadokeza ishara ya kuhusika na hatima ya Irak, mkakati ambao si muhimu sana kwa rais George W.Bush. Msimamo wa busara zaidi ni ule wa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, wa kupinga mazungumzo pamoja na wahalifu, ili pasije pakafanyika kosa lingine kama lile la wakati wa kuvamiwa Irak.
Gazeti la mji wa mashariki wa Chemnitz, FREIE PRESSE kuhusu nakisi iliyotokea katika bajeti ya matumizi ya ndani katika Ujerumani ya zaidi ya Euro Bilioni 43, linaandika: Anayekadiria hali kwa maniki anatambua kwamba, wala waziri wa fedha Eichel wala chama fulani cha kisiasa kulaumiwa pekee.
Mzigo huu wa nakisi ni kosa la tangu muda mrefu, hata kabla ya Kansela Schröder na washirika wake kuingia madarakani.
Gazeti la kusini mwa Ujerumani STUTTGARTER ZEITUNG, linachangia mada hii kwa kuandika: Hii ni rekodi ya kusikitisha mno. Haiba ya zamani ya waziri Eichel kama mtaalamu wa mambo ya pesa, imeathirika. Lakini inabidi kukumbukwa kwamba, nakisi hii haitokani na udhaifu wa waziri Eichel, bali mzigo huu wa madeni unatokana na kuzidi kudidimia maendeleo ya kiuchumi katika Ujerumani tangu miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo waziri Eichel hakujifunza chochote kutokana na hali hiyo, bali anaendeleas na mtindo wake wa kawaida wa kutoa ahadi, ambazo hawezi kutekeleza.
Gazeti mashuhuri la mji mkuu Berlin, DIE WELT, linapojishughulisha na mpango wa kuliokoa shirika mojawapo mashuhuri la maduka katika Ujerumani la Karlstadt-Quelle, linaandika: Mzozo wa shirika hili na hangaiko iliyotokea, ni mfano mwema wa jinsi hali ilivyo kwa jumla katika Ujerumani. Kila mwenye biashara dogo ya maduka, anajua tangu muda mrefu jinsi maduka makubwa ya Ujerumani yanavyokabiliwa mfululuzo na mzozo wa kibiashara.
Mara nyingi inazungumzwa juu ya siasa za biashara, lakini matokeo yake karibu hayahisiwi. Chama cha watumishi wa huduma za kijamii Verdi, ambacho kimebeba dhamana ya kuliokoa shirika hili, kinajua tangu muda mrefu, hali nyonge ambayo imekuwa ikiibana Karlstadt-Quelle. Katika Ujerumani yanazungmzwa mengi badala ya kuchukuliwa hatua.