Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo
1 Novemba 2004Gazeti la mashariki mwa Ujerumani LAUSITZER RUNDSCHAU, kuhusu mjadala wa kutafuta njia ya kuwapatia au kutowapatia nyongeza ya misaada ya pesa wastaafu, linaandika: Tangu muda mrefu bima ya malipo ya uzeeni haikuwahi kuwa madhubuti, hadi pale yalipofanyika mageuzi yaliyojulikana ya Riester miaka mitatu iliyopita. Mara kwa mara utaratibu wa malipo hayo husahihishwa, na inaelekea mnamo mwaka huu wastaafu hawatapata nyongeza hiyo ya malipo, hali ambayo pia itawabebesha mzigo wa kutopata huduma za wasiojiweza. Mpango wa sasa ni kwamba, kuanzia mwaka ujao wa 2005, malipo ya uzeeni yatakuwa yakipimwa na kulipwa kulingana na mishahara ya wakati wa kufanya kazi. Ndio maana serikali itafanya kosa kubhwa, iwapo inawatolea ahadi wastaafu ambazo haiwezi kutekeleza.
Gazeti lingine la mashariki MITTELDEUTSCHE ZEITUNG, kuhusu kashfa iliyogunduliwa kwenye wizara ya usafiri ya Ujerumani, linaandika: Vyama vya upinzani katika mbunge mjini Berlin, vinadai kwa kauli moja kufanyika uchunguzti kinaganaga kuhusu kashfa hii ya rushwa.
Msemaji wa kundi la chama-tawsala SPD, Klaas Hübner, kuhusu mashkata haya alisema katibu wa dola kwenye wizara ya usafiri, Ralf Nage, ameashatayarisha faili yenye orodha ya wale wote wanaoshukiwa kuhusika na kashfa hiyo. Angependa ripoti hiyo ichunguzwe kwa mjadala katika bunge. Msemaji wa maswala ya usafiri wa vyama-ndugu vya upinzani Klaus Lippold, naye anadai ripoti hiyo iwekwe mezani bila ya kuchelewa, hataki iwekwe katika makabati hadi baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2006. Anatumai waziri mhusika Manfred Stolpe atachukua hatua inayohusika haraka iwezekanavyo.
Gazeti la kusini mwa Ujerumani FRANKFURTER RUNDSCHAU, kuhusu kitisho cha mashambulio ya wafuasi wa utando wa al-Kaida linaandika: Siku nne kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais nchini Marekani, kiongozi wake, ameutumia risala maalum umma wa marekani. Osama bin Laden, hakuchukua hatua hii makusudi, lakini huenda ikawa mchango wa kumuunga mkono rais wa sasa Georg W.Bush. Kwa maneno mengine gaidi huyu mkubwa kabisa anayetafutwa kote duniani, amegeuka ghafla ni msaada na wakati muafaka kwa rais Bush. Lakini hata kwa idara ya upelelezi ya Marekani CIA video yenye risala hiyo si hakika kabisa. Ijapokuwa hayo kitisho hiki wakati wa kufanyika uchagtuzi, kisije kikapuuzwa, kwa sababu wagombea wote wawili wa wadhifa wa rais, hawawezi kuliumbia macho mbele ya wapigaji kura wao.
Tunakamilisha uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo, kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti la MITTELDEUTASCHE ZEITUNG kuhusu mkutano mkuu wa chama cha upinzani cha PDS, linasema: Sasa wasoshalisti wananuwia kukabiliana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2006 kwa mikakati mipya, ili kuwavutia wapigaji kura wao. Lengo lao mojawapo ni kuhakikishwa haki sawa katika huduma za kijamii, kwa kuwatoza kodi kubwa zaidi kwa matajiri na wale wanaopata mishahara minono, isitoshe, kwa kusimamiwa bora zaidi mfumo wa uchumi na serikali. Tutumai tu kwamba, haitasahauliwa umuhimu wa kusimamiwa kwa uchumi chini ya mikakati ya kisoshalisti.