Uchambuzi wa magazeti ya Ujerumani hii leo
2 Novemba 2004Afrika Kisahili 02.11.04 M.A.Rukungu
Gazeti la kusini mwa Ujerumani FRANKFURTER RUNDSCHAU, kuhusu uchaguzi wa rais nchini Marekani hii leo, linaandika: Mahusiano ya kisiasa kati ya nchi za ulaya pamoja na mgombea mpya wadhifa wa rais John Kerry ni wenye kina kirefu zaidi kupita yale na rais wa hadi sasa George W.Bush. Mahusiano haya yatapata nguvu mpya endapo Mdemokrat Kerry atathibitisha kipaji chake cha kutatua maswala ya siasa za ndani na za nje, kupita mshindani wake Bush. Nao mashehe wa Teheran watataka kumfanyia mtihani wa kutokawia sana katika kuwachukulia hatua viongozi wenye vichwa vigumu wa Korea ya Kaskazini, wapiganaji wa chini kwa chini nchini Irak na kumtafuta na kumtia mbaroni Osama bin Laden. Haya yangekuwa ni kwa masilahi ya nchi za ulaya, na hii ingekkuwa ni fursa ya Kerry kujiimarisha katika siasa za kimataifa.
Nalo gazeti la mji wa Heidelberg RHEIN-NECKAR-ZEITUNG, linakumbusha: bila kujali jinsi matokeo ya uchaguizi wa rais nchini Marekani yatakavyokuwa, hili ni swala ambalo lisingetupita vivi hivi. Kwa Bw.Bush, ambaye hadhi yake imeumia sana kutokana na vita vya Irak, yote yangebakia kama yalivyo sasa.
Kuhusu Bw.Kerry kwa bara la ulaya linabakia swali muhimu, jinsi angalivyoweza kukabiliana na shuguli za kijeshi, na sio kuhusiana na Irak pekee.
Gazetzi lingine mashuhuri la kusini mwa Ujerumani FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG, linatupia macho matokeo ya kwanza ya rais nchini Ukraine na kuandika: Wafuasi wa rais wa hadi sasa Kutschma, pamoja na wawakilishi wa vyombo vya kushawishi uchaguzi huo vya kiRussia, watachukua kila hatua itakayowezekana kuhakikisha kwamba, hatamu za uongoni katika Kiev, zitakuwa mikononi mwa mgombea anayeungwa mkono na serikali ya Moscow. Baada ya hapo serikali ya Moscow itaridhika kuwa na washirika wanaowafaa: Lukaschenka katikia Minsk, Janukowitsch katika Kiev na Putin katika Moscow.Washirika wa Moscow katika magharibi: Ujerumani, Ufaransa na makao makuu ya umoja wa ulaya mjini Brussels, itawabidi kuonyesha kama wanaridhika kwa kutonyamaza kimya. Bado hawakuchelewa kutangaza maoni na kuchukua hatua zao kuhusu matokeo ya uchaguzi huo, kwamba wanajipanga katika upande wa mwenye kuidhinisha mageuzi katika Kiev.
Gazeti la BADISCHE TAGBLATT, linachangia mada hii kwa kuandika: Tangu miezi viongozi katika Kiev wanazungumzia juu ya kuigwa mtindo wa mtawala wa kiimla katika Beroruss Alexander Lukaschenko. Sababu ni kwa kuwa anaendelea kuukandamiza mfululizo upande wa upinzani, haruhusu uchaguzi wa haki na kila mara anatafuta namna ya kupalilia mahusiano ya karibu pamoja na Russia. Uamuzi kama Ukraine itashika njia kuelekea ulaya, chini ya uongozi wa Juschtschenko, utapatikana baada ya kufanyika duru ya pili ya uchaguzi katika wiki mbili zijazo.
Tunakamilisha uchabuzi wetu wa leo kutoka magazeti ya Ujerumani, kwa kutazama yale yanayoandikwa na gazeti la kibisahara HANDELSBLATT kuhusu kashfa ya rushwa iliyogunduliwa kwenye wizara ya usafiri ya Ujerumani
linakumbusha: Bado inakosa sheria maalum katika Ujerumani ya kupambana na rushwa, na bado zinakosa kanuni za kisheria za kuwachukulua hatua wale maofisa wanaokubali kuhongwa. Si hayo tu, bali pia inakosa jitihada ya kuchukuliwa hatua rahisi kabisa za kupiga vita rushwa kwa jumla.