Uchaguzi wa Ujerumani na sera za uchumi
23 Septemba 2009Athari za msukosuko wa fedha ulimwenguni tangu miezi kadhaa, zimeikumba pia Ujerumani.Ingawa kumechomoza ishara za kwanza hivi punde hali inaanza kupambazuka,hatahivyo, mawingu bado yametanda na hakuna awezae kubashiri iwapo kweli hali ya uchumi inapambazuka.
Kampeni ya uchaguzi ya mwaka huu 2009, inakwenda tofauti kabisa na ile ya mwaka 2005 ambayo iliongoza Kiongozi wa chama cha (CDU ) Bibi Angela Merkel , kuibuka Kanzela wa Ujerumani.
"Kila kipindi kina jukumu lake. Mwaka 2005 , tulikuwa katika hali bora zaidi ya kiuchumi na tulikuwa na bajeti iliovuka mpaka kimatumizi.Ilitupasa kusaifisha hazina na sio kutokana na msukosuko wa fedha ulimwenguni uliozuka.Msukosuko huwa haukumalizika unapokuwa umerekebisha nakisi na kuiweka sawa , bali unamalizika, unaporudi katika hali uliojikuta kabla ya msukosuko kutokea.Shabaha sasa ni kuzitia jeki nguvu za ukuaji uchumi; na kufikia shabaha hiyo kuna tofauti kubwa kati ya sera za vyama mbali mbali."
Ikiwa mtu atakisadiki chama cha Social Democratic Party (SPD) kisemavyo, tofauti hizo daima zimekuwapo.Lakini,msukosuko wa Opel,Karstadt,Hypo Real Estate- ni ya nadra. Mtetezi wa wadhifa wa ukanzela wa chama hicho cha SPD,waziri wa nje Bw.Frank-Walter Steinmeier, anathibitisha kuwa katika serikali yao ya muungano wa vyama vikuu waliafikiana haraka suluhisho:
"Nikitupia macho nyuma miezi 7 hadi 8 iliopita , tulipojikuta kwenye msukosuko,takriban mara nyingi mno, mbinu na mashauri zilitoka chama cha SPD.Zilitolewa na mawaziri wa chama cha SPD kama yule wa fedha Steinbrück, waziri wa kazi Scholz, waziri wa nje Steinmeier ambao walishughulikia kutungwa mpango wa kuufufua uchumi,ule wa kuekeza raslimali uliotuwezesha kurefusha nafasi za kazi za vipindi vifupi.Mashauri hayo yote, yalitoka chama cha SPD ambayo tuliyapitisha licha ya kukosolewa ndani ya serikali ya muungano."
Swali linaloibuka ni hili: Kwa umbali gani serikali iingilie maswali ya uchumi? Je, wanasiasa ni wanabeki bora kuliko wanabenki na mameneja wake ?
Je, mlipakodi anastahiki kulipia gharama za madhambi wafanyayo vigogo vya makampuni ? Msaada wa kifedha wa serikali usipindukie kima gani katika kuyaokoa mabenki na makampuni yaliofilisika ?
Ulipozuka msukosuko wa Hypo Real Estate-Banki ya mikopo ya nyumba, maswali yote hayo ghafula yalichomoza.Kuporomoka kwa Banki hiyo mwishoni mwa 2008 , kuliibua msukosuko mkubwa wa uchumi nchini Ujerumani.Kwahivyo, serikali ya Ujerumani ikaamua kuitaifisha banki hiyo.Banki hii imebaki hayi kwa kuwa serikli ya shirikisho na banki nyenginezo , zilitoa kiinua-mgongo cha dhamana ya fedha cha kiasi cha Euro bilioni 100.Je, huo ulikuwa uamuzi sahihihi ?
Kwa muujibu wa waziri wa fedha Steinbrueck, swali wakati ule, halikuwa kuiokoa banki hiyo,bali kuzuwia mfumo mzima wa fedha nchini Ujerumani na athari zake kubwa kuporomoka.
Mtayarishi: Kinkartz Sabine/ZR/Ramadhan Ali
Mhariri:Abdul-Rahman