Uchaguzi wa Rais kurudiwa Iran
18 Juni 2005Matangazo
Tehran:
Uchaguzi wa rais nchini Iran utafanywa tena. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Iran, hakuna hata mgombea mmoja, kati ya saba, aliyepata wingi mkubwa. Kwa hiyo, kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Iran, uchaguzi utarudiwa Ijumaa ijayo. Kwa mujibu wa matokeo ya awali, mgombea anayependwa sana, Rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani, anaongoza akifuatiwa na Mhafidhina Meya wa Tehran Mahmud Ahmadineshad. Asili mia 60 ya wapiga kura wamepiga kura. Kutokana na msongamano uliotokea wakati wa kupiga kura ilibidi muda wa kupiga kura uongezwe kwa ghafla. Upigaji kura wa jana ulijionea ulinzi mkali baada ya mashambulio ya mabomu kuzagaa nchini kote.