Uchaguzi Saudi Arabia.
10 Februari 2005RIYADH:
Wanaume nchini Saudi Arabia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Mabaraza ya Miji ambao unawanyima nafasi wanawake ya kupiga kura.
Ni wanaume 148,000 tu wakiwa wanawakilisha asilimia 37 ya watu 400,000 wenye uwezo wa kupiga katika mji mkuu Riyadh pamoja na vitongoji vyake wamejiandikisha kupiga kura zao,huku wanaume wengi nchini humo wakiwa hawaridhishwi na mwenendo wa upigaji kura huo.
Ingawa taratibu za upigaji kura nchini Saudi Arabia hazielezi chochote juu ya nafasi ya wanawake ambao wanafanya idadi ya zaidi ya nusu ya raia wote wa Saudi Arabia,Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Prince Nayef bin Abdul Aziz amepinga ushiriki wao katika kuchagua.
Uchaguzi huo ni katika muelekeo wa hatua za kufanya marekebisho kiasi ambapo serikali ya Saudi Arabia inasisitiza kuwa ni kwa ajili ya kukidhi matakwa yake na sio shinikizo kutoka mataifa ya Magharibi.