Uchaguzi Mkuu Tanzania kufanyika Oktoba 29
26 Julai 2025Matangazo
Tangazo hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma.
Kulingana na Mwambegele, kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 27, itakuwa ni kipindi cha kampeni. Jumla ya wapigakura waliojiandikisha ni milioni 37.65.
Tanzania inafanya uchaguzi mkuu wa 2025 huku kukiwa na shinikizo la kudai marekebisho ya sheria za usimamizi uchaguzi, na chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kikisusia kushiriki uchaguzi huo.