You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Mzozo wa Kongo Mashariki
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Uchaguzi Mkuu Kenya 2017
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Ujerumani yaisaidia Afrika Mashariki katika mambo muhimu
Ujerumani yaisaidia Afrika Mashariki katika mambo muhimu
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta asema Afrika iko njia panda
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta asema Afrika iko njia panda
Kenya kuiondoa miraa kwenye orodha ya dawa za kulevya
Kenya imesema itaiondoa miraa kwenye orodha ya dawa za kulevya, miaka mitatu ijayo kwa kukosa ushahidi wa kisayansi.
Polisi 20 Kenya wameuawa ama walijiua tangu Januari 2021
Takwimu za Shirika Huru la Kutetea Haki za waathiriwa Kisheria na Kimatibabu la IMLU nchini Kenya zinaonesha kuwa maafisa 20 wa polisi wameuawa ama walijiua tangu mwezi Januari mwaka 2021. Shisia Wasilwa anaripoti zaidi.
Rais Kenyatta aamrishwa kuwateua majaji katika siku 14
Mahakama Kuu Kenya imemuagiza Rais Uhuru Kenyatta kuwateua na kuwaapisha majaji 6 katika orodha iliyowasilishwa kwake na Tume ya Mahakama nchini humo JSC katika siku 14 zijazo. Iwapo Kenyatta atafeli kufanya hivyo ndani ya muda huo, Mahakama Kuu imeagiza kuapishwa kwa majaji hao na waanze majukumu yao mapya mara moja. Sikiliza mahojiano ya Saumu Njama na wakili wa kikatiba Justus Munyibia.
Kenya yaondoa marufuku ya kutembea usiku
Rais Uhuru Kenyatta ameondoa marufuku ya kutembea usiku ambayo imekuwepo tangu mwaka 2020.
Mume wa mwanariadha wa Kenya Agnes Tirop akamatwa na polisi
Mshukiwa wa mauaji ya mwanariadha wa Kenya,Agnes Tirop,amekamatwa na atafikishwa mahakamani hivi karibuni yasema polisi.
Wazee wanaotuhumiwa kuwa wachawi
Maisha ya wazee katika baadhi ya sehemu huko pwani ya Kenya yako hatarini kutokana na dhana ya vijana kwamba wazee hao ni washirikina na wachawi. Vijana hao aghalabu husema wazee hao ndio wahusika wakuu wa kutofanikiwa kwao maishani. Thelma Mwadzaya analivalia njua suala hili katika makala ya Mbiu ya Mnyonge.
Mshindi wa medali ya mashindano ya dunia Kenya Tirop afariki
Mwanariadha Agnes Jebet Tirop akutwa amefariki katika kisa kinachodaiwa kuwa mauaji.
Rais Kenyatta alaani uamuzi wa ICJ kuhusu mzozo na Somalia
Kenya imepuuzilia mbali uamuzi uliotolea na Mahakama ya Haki ya Kimataifa ICJ kuhusu mpaka wake na Somalia kwenye bahari ya Hindi. Rais Uhuru Kenyatta amelaani uamuzi huo akisema kuwa Kenya haitakubali kamwe unyakuzi wa ardhi yake. Kwa upande wake Somalia imepongeza hatua hiyo baada ya Mahakama ya ICJ kuipa kipande kikubwa cha eneo hilo linalozozaniwa na mataifa hayo.
ICJ yaiunga mkono Somalia katika mzozo na Kenya
Eneo la bahari linalozozaniwa linadaiwa kuwa na utajiri wa gesi.
Mpango wa Kenya kuwanusuru wafugaji dhidi ya maafa ya ukame
Serikali ya Kenya ilizindua mpango wa kununua mifugo kutoka kwa wafugaji kama njia ya kuwasaidia kukabiliana na hali ya kiangazi inayoshuhudiwa kwa sasa nchini humo, huku makundi mengine ya watu katika jamii yakionekana kama yameachwa kando. Sudi Mnette amezungumza na Naibu Gavana wa Jimbo la Marsabit, Solon Riwe, kuhusu mpango huo. Ameanza kwa kueleza namna watakavyofaidika na mpango huo.
ICJ kuamua kuhusu mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia
Mahakama ya Kimataifa ya Haki-ICJ itatoa uamuzi wake Jumanne kuhusu mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia.
Kenya kuwasaidia wafugaji wake kukabiliana na kiangazi
Serikali kutumia jumla ya shilingi milioni 450 kusaidia majimbo kumi yaliyo katika hatari ya kupozeteza mifugo yao.
Balozi zakanusha kushawishi chaguzi Kenya
Afisi za ubalozi wa Uingereza, Ujerumani na Canada nchini Kenya zimekanusha kuwepo kwa mpango wowote wa kumpendelea mgombea mmoja wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Kenya. Tangazo la balozi hizo linaonekana kama kukanusha madai yaliyotolewa na mwanasiasa mmoja nchini humo, aliyesema jumuiya ya kimataifa ina ushawishi mkubwa katika kumchagua kiongozi wa Kenya. Sikiliza ripoti ya Wakio Mbogho.
Maadhimisho ya siku ya walimu ulimwenguni
Ulimwengu unaadhimisha siku ya walimu ulimwenguni. Kauli mbiu ya mwaka huu inajikita kwenye juhudi za kuwaunga mkono na kuwapiga jeki walimu ili kufanikisha mchakato wa kurejea kwenye maisha ya kawaida kufuatia misukosuko ya COVID 19. Nchini Kenya walimu wanapitia kipindi tofauti hasa baada ya mtaala wa shule kufanyiwa mabadiliko makubwa.
Kituo kingine cha forodha katika mpaka wa Kenya na Uganda
Hatua hiyo itasaidia kupunguza muda unaochukuliwa kwenye forodha zilizoko kwa sasa mpakani baina ya nchi mbili hizi.
KANU yamteua Gideon Moi kuwania urais Kenya 2022
KANU yamwidhinisha Gideon Moi kuwania urais Kenya 2022
Kenya yazuia filamu nyingine ya mapenzi ya jinsia moja
Kwa mara ya pili serikali ya Kenya imepiga marufuku filamu inayoangazia masuala ya mapenzi ya jinsia moja iitwayo “I am Samuel”. Bodi ya filamu KFCB ilitangaza kuwa filamu hiyo haifai kutazamwa na wakenya kwani inakiuka maadili na katiba. Filamu hiyo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mwezi wa Oktoba mwaka jana kwenye tamasha la 64 la filamu la London, BFI.
Watu saba wamekufa kwa ajali ya boti Kenya
Afisa moja nchini Kenya amesema watu saba wamekufa baada ya boti yao kuzama katika ziwa Victoria.
Kenya yatenga shilingi bilioni 2 kupambana na njaa
Serikali ya Kenya yaanza kutuma misaada kwa wafugaji ambao wanakabiliwa na njaa kufuatia ukame.
Visa vya ajali vyaongezeka Kenya mwaka 2021
Utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Usafiri na Usalama nchini Kenya NTSA, unaonesha zaidi ya watu 3,000 wamekufa nchini humo kutokana na ajali za barabarani tangu kuanza kwa mwaka 2021. Ikilinganishwa na mwaka uliopita, idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 25 ya vifo vilivyosababishwa na ajali za barabarani nchini Kenya. Sikiliza ripoti zaidi kutoka kwa mwandishi wetu Shisia Wasilwa.
Dira ya kitaifa ya Kenya ya 2030 imefikiwa au la?
Raia nchini Kenya wana shauku ya kufahamu iwapo malengo ya mpango wa maendelo wa mwaka 2030 yatafikiwa katika wakati ufisadi na siasa za uhasama zikitajwa kama vikwazo kwa Kenya kupiga hatua. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Wakio Mbogho kutoka Nakuru.
Watu 8 waliozama ziwa Victoria Kenya waendelea kutafutwa
Waliofariki katika ajali ya mashua Ziwa Victoria, Homabay Kenya wafikia watatu baada ya mwili mmoja kupatikana Jumatano.
Wito wa amani watolewa katika maeneo yenye mizozo Kenya
Kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani ya mwaka huu nchini Kenya, wadau mbalimbali wamehimizwa kuhakikisha kunakuwepo mazungumzo ya uwazi katika kuelewa vyanzo vya machafuko ili kujenga jamii zilizo na uthabiti, haki na usawa. Taifa hilo limeshuhudia matukio ya jamii kuzozana. Licha ya juhudi za amani matatizo yameendelea kushuhudiwa. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Wakio Mbogho.
HRW: Wahanga wa ukatili wa kijinsia wakosa msaada Kenya
Wanawake wanaoishi katika lindi la umaskini wameathirika zaidi wakati wa janga la Corona
Jaji asema polisi nchini Kenya wana kesi ya kujibu
Jaji asema polisi wana kesi ya kujibu kuhusu mauaji ya wakili wa haki za binaadamu nchini Kenya.
Ruto tayari kuzungumza na Kenyatta bila masharti
Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini Kenya wamewataka Ruto na Kenyatta kuzika tofauti zao kufuatia uhasama wa miezi mingi.
Bei ya mafuta yapanda maradufu nchini Kenya
Bei ya mafuta yapanda maradufu nchini Kenya
Athari za ukame Tana River, Kenya
Ukame unaoendelea kulikumba jimbo la Tanariva katika Pwani ya Kenya umeathiri vibaya shughuli za masomo ambapo kwa sasa mamia ya wanafunzi hawaudhurii shule kwa sababu ya kuhama kwenda kutafuta maji. Faiz Musa na taarifa kamili.
Maswali yaibuka kuhusu miili 11 ilopatikana Mto Tana Kenya
Viongozi wataka serikali ya Kenya kutoa majibu kuhusu miili iliyogunduliwa Mto Tana
Mwanamke wa kwanza kuteuliwa askofu wa Kianglikana Kenya
Uteuzi wa mwanamke kuwa askofu waibua hisia mseto Kenya.
Tathmini kuhusu hali ya ukame nchini Kenya
Kufuatia hali ya ukame nchini Kenya ambao tayari umeshatangazwa na Rais Kenyatta kuwa janga la kitaifaTatu Karema amezungumza na Profesa Hamadi Boga, katibu katika wizara ya kilimo kutathmini hali halisi. Kwa mengi zaidi, sikiliza mahojiano.
Rais Kenyatta atangaza ukame kuwa janga la kitaifa Kenya
Wakenya milioni mbili kutoka majimbo 10 wanakabiliwa na ukame.
Wabunge wawili wazuiliwa kuhusiana na machafuko Laikipia
Duru nchini Kenya zinasema polisi inawahoji wabunge wawili kuhusiana na machafuko yanayojitokeza huko kaunti ya Laikipia ambako makundi yenye silaha yanaendesha hujuma dhidi ya raia na kupambana na maafisa wa usalama. Rashid Chilumba amezungumza na kamishna wa jimbo la Bonde la Ufa anayesimamia pia kaunti ya Laikipia George Natembeya na kwanza alitaka kujua wamefikia wapi kwenye mahojiano hayo.
Hali ni tete huko Laikipia, Kenya
Makabiliano makali kati ya polisi na kundi la watu wenye silaha yameshuhudiwa usiku wa kuamkia leo katika eneo la
Onyo la Baraza la Waandishi wa Habari kwa wanasiasa wa Kenya
Mitandao ya kijamii inatumiwa na wanasiasa kuvipiga vita vyombo vya habari na kuwarai umma kususia kuvifuatilia Kenya.
Muungano mpya wa siasa wazinduliwa nchini Kenya
Wanasiasa kadhaa Kenya,wamejiunga katika walichokiita ''Muungano wa Wazalendo'' watakachokitumia kuwania kiti cha urais.
Wanyamapori wasafirishwa kikatili kutoka Afrika
World Animal Protection imefichuwa uhalifu wa kuwakamata na kuwasafirisha wanyama pori kikatili kutoka Afrika.
Trachoma mjini Kajiado, Kenya
Hofu ya ugonjwa wa Tracom huko kajiado nchini Kenya inazidi kuongezeka mno. Hii ni kutokana na mazingira yanayosababisha ongezeko la viini vinavyosababisha ugonjwa huo. Sikiliza makala ya afya yako iliyoandaliwa naye Shisia Wasilwa ambaye aliutembelea mji huo na kukutana na wanaougua ugonjwa huo.
Makamu wa Rais wa Kenya aapa kutojiuzulu
Makamu wa rais wa Kenya William Ruto amesema kamwe hatojiuzulu
Rais Kenyatta amtaka makamu wake William Ruto kujiuzulu
Rais huyo ameeleza kuwa hafahamu kwa nini makamu wake ameamua kumshambulia kila mara, badala ya kuachia madaraka,
Bishara yaimarika Jumuiya ya EAC licha ya COVID19
Biashara kati ya Kenya na Tanzania imeongezeka mara sita zaidi katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita
Mahakama ya rufaa Kenya kuamua kuhusu mageuzi ya katiba
Uamuzi kuhusu mchakato wa kuibadilisha katiba ya Kenya kupitia mpango wa BBI unaosubiriwa kwa hamu kutolewa leo Ijumaa.
Mahakama yasitisha marufuku ya mikutano ya kisiasa Kenya
Mahakama Kuu imesitisha kwa muda marufuku ya mikutano ya kisiasa kama njia ya kuzuwia corona kusambaa.
Upinzani Kenya wahakikisha kuwa na mgombea mmoja wa urais 2022
Uongozi wa Muungano wa Kenya Moja-OKA unaovijumuisha vyama vinne nchini Kenya umesema kuwa utakuwa na mgombea mmoja wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2022. Hata hivyo Uongozi wa Muungano huo ulikosa kumtaja kiongozi ambaye atakayepeperusha bendera ya muungano huo ukishikilia, kuwa utafanya hivyo wakati mwafaka.
Walimu Kenya wapewa siku 7 kupata chanjo
Licha ya kupewa kipau mbele katika zoezi la kutoa chanjo ya COVID 19, ni asilimia 33 ya waalimu nchini Kenya pekee waliopata chanjo hii kikamilifu. Serikali hiyo sasa imetoa muda wa siku saba kwa waalimu wote kupata chanjo la sivyo waadhibiwe. Isikilize ripoti ya Wakio Mbogho.
Muungano mpya wa kisiasa waundwa Mlima Kenya
Wanasiasa watatu wa eneo la Mlima Kenya Martha Karua wa NARC Kenya, Mwangi Kiunjuri wa Chama cha Huduma na Moses Kuria wa Chama cha Kazi wametangaza kuunda muungano mpya wa kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.
Kenyatta ampigia upatu Odinga kumrithi 2022
Kwanini rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anampigia upatu kiongozi wa upinzani Raila Odinga kumrithi mwaka 2022?
Uhusiano tata kati ya Kenya Uganda
Vita vya maneno vimekuwa vikiendelea kati ya pande za kisiasa nchini Kenya na Uganda kuhusiana na hatua ya naibu wa rais Kenya William Ruto kuzuiwa kusafari kuelekea Uganda. Kupata picha kamili kuhusu cheche hizo za maneno na athari yake kwenye uhusiano baina ya mataifa hayo mawili, Tatu Karema amezungumza na Martin Oloo mchambuzi wa kisiasa kutoka Kenya na kwanza anaelezea tofauti zilizopo.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 8 wa 23
Ukurasa unaofuatia