Uchafuzi wa hewa huchochea saratani ya mapafu
4 Februari 2025Matangazo
Watu milioni 2.5 waligunduliwa kuwa na saratani hiyo ya mapafu mnamo mwaka 2022. Takwimu hizi ni kulingana na utafiti huo uliochapishwa katika jarida la tiba ya Lancet Respiratory Medicine, kuhisiana na Siku ya Saratani Duniani.
Wengi wa waliogunduliwa walikuwa ni wanaume, ingawa kuligundulika ongezeko la karibu visa milioni moja miongoni mwa wanawake.
Saratani inasababisha vifo zaidi duniani
Utafiti huo umeonyesha aina moja ndogo ya saratani ya mapafu ya adenocarcinoma ambayo ndio imewaathiri zaidi wanawake katika nchi 185.