Mtaa wa mabanda wa Kibera ulioko mjini Nairobi umekuwa moja ya nguzo ya ubunifu barani Afrika. Katika mazingira yenye changamoto, wakaazi wa mtaa huo wamekumbatia mradi wa kuchakata taka za plastiki kama njia ya kuleta mabadiliko chanya. Kwa kila kilo ya plastiki, wanapokea "Green Points" zinazoweza kutumika kulipia huduma muhimu kama maji safi ya kunywa, vyoo vya kuoga na kupata chakula.