Ubeligiji yataka kesi ya mmisionari Theunis ikasikilizwe Brussels.
27 Septemba 2005Matangazo
Brussels:
Serikali ya Ubeligiji imeanza utaratibu wa kutaka mmisionari aliyekamatwa nchini Rwanda Guy Theunis ,arejeshwe Ubeligiji na kuhakikisha kesi inayomkabili ya maovu dhidi ya binaadamu inasikilizwa nyumbani. Mahakama ya kijadi ya Gachacha nchini Rwanda ilimfungulia mashitaka mmisionari huyo wa Kibeligiji, ya kuchochea na kupanga mauaji ya halaiki ya 1994 ambapo zaidi ya watu laki tano waliuwawa. Kesi yake ilipelekwa moja kwa moja kwa mahakama ya kawaida ambako atakabiliwa na adhabu ya kifo pindi akipatikana na hatia.