Ubelgiji yasema hali nchini Kongo bado haijaimarika
20 Agosti 2025Matangazo
Wakati wa ziara nchini Kongo, Prevot amesema Ubelgiji ilikuwa na imani katika mchakato wa amani unaoendelea kati ya pande hizo mbili, chini ya upatanishi wa Qatar, lakini mwezi mmoja baadaye, hali nchini humo haijaimarika.
Uingereza na Ubelgiji zalalamikiwa kwa machafuko ya DRC
Katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na spika wa bunge wa Kongo Vital Kamerhe, Prevost amesema vitendo vingi vya ukatili na mauaji yamefanyika mashariki mwa Kongo na akatoa wito wa kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha vita.
Waziri huyo yuko katika ziara barani Afrika iliyoanza katika taifa jirani la Jamhuri ya Kongo, ambapo pia atatembelea Kenya na Ethiopia.