Ubelgiji yakosoa hatua ya Rwanda kuunga mkono waasi wa M23
27 Aprili 2025Katika mahojiano na shirika la habari la AFP, Prevot amezihimiza pande zote mbili katika mzozo huo wa Kongo kujadiliana ili kuumaliza mzozo kwenye eneo la mashariki lenye machafuko nchini humo ambapo waasi wa M23 wameteka maeneo mengi kutoka kwa serikali.
Baada ya kukutana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni siku ya Ijumaa mjini Kampala, Prevot aliiambia AFP kwamba hakutakuwa na suluhisho la kijeshi mashariki mwa Kongo na kwamba wanahitaji mazungumzo.
Soma pia: Kongo na M23 watangaza kusitisha mapigano
Pevot amesema hali katika eneo hilo bado ni mbaya sana na wakaazi wanapitia mateso kila siku.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Ubelgiji pia ameelezea wasiwasi wa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu na kusema kuna haja ya dharura ya kuchukuliwa kwa hatua.