Uamuzi wa mahakama wazua mashaka kwa wafanyakazi wa VOA
5 Mei 2025Hayo ni baada ya Rais Donald Trump kulifunga mnamo mwezi Machi. Shirika la VOA linaloendeshwa na serikali ya Marekani kwa ajili ya kutoa huduma ya Habari duniani kote, limekuwa halipatikani hewani tangu Trump alipoamuru kuvunjwa kwa asasi kuu ya kimataifa ya vyombo vya Habari, USAGM. Asasi hiyo inasimamia shirika la VOA na vituo vingine ikiwa ni pamoja na Radio Free Asia na ndiyo inayotoa ufadhili wa fedha kwa matawi hayo yote.
Soma pia: Marekani: Mashirika ya habari yanayofadhiliwa na serikali yasimamishwa
Majaji wawili walioteuliwa na Trump, wamesema katika uamuzi wao kwamba yumkini mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kuyashughulikia masuala ya wafanyakazi wa USAGM. Jaji wa tatu, Cornelia Pillard, aliyeteuliwa na rais wa zamani Barack Obama, amepinga uamuzi huo. Rais Trump ameuliza kwa nini shirika hilo linalotangaza kwa mamilioni ya wasikilizaji na watazamaji duniani haliwakilishi mtazamo wa utawala wake.