Tuzo za Balon D'or kufanyika Septemba 22
19 Mei 2025Matangazo
Hafla ya tuzo ya Ballon d'Or zimetangazwa kuwa zitafanyika Septemba 22 mwaka huu na idadi ya tuzo kwa wanawake na wanaume zitakuwa sawa kwa mara ya kwanza, waandaaji wamesema leo jumatatu.
Tuzo za mlinda mlango bora wa wanawake, mchezaji bora wa kike na mfungaji bora wa wanawake katika klabu au timu ya taifa zimeongezwa kwenye orodha mwaka huu katika sherehe hizo zitakazofanyika mjini Paris, gazeti la France Football na UEFA limesema.
Walioteuliwa katika tuzo hizo watatangazwa mapema mwezi Agosti.