Tunisia yakosoa ripoti ya UN kuhusu ukandamizaji
25 Februari 2025Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za binadamu iliituhumu nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika kwa "kuwaaandama wakosoaji wake wa kisiasa" ikiwemo ukamataji wa mabavu, kuwafungulia mashtaka na kuendesha kesi kinyume cha utaratibu dhidi ya wanaharakati, waandishi habari na wanasiasa wa upinzani.
Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Tunisia imeyapinga madai hayo kwenye tamko lake ililolitoa kupitia ukurasa rasmi wa Facebook usiku wa kuamkia leo.
Imesema imeshangazwa sana na ukosoaji huo wa Umoja wa Mataifa uliojumuishwa kwenye tamko la Mkuu wa Haki wa Binadamu wa Umoja wa Umoja. Taarifa hiyo imesema Tunisia haioni haja ya kuelezea jinsi ilivyodhamiria kulinda haki za binadamu kwa sababu inaamini juu ya umuhimu wa haki hizo ambazo zinalindwa chinia ya katiba na sheria za nchi hiyo.
Ukosoaji wa Umoja wa Mataifa unafuatia matukio yaliyofuatia uamuzi wa Rais Kais Saied wa Tunisia wa mwaka 2021 wa kujipatia madaraka makubwa kupitia mabadiliko ya katiba.