Tshisekedi: Mkataba wa amani na Rwanda ni wa kihistoria
30 Juni 2025Matangazo
Felix Tshisekedi ameitoa kauli hiyo leo wakati nchi yake ikiadhimisha miaka 65 tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni Ubelgiji , kumbukumbu ambayo inafanyika wakati huu kukishuhudiwa mizozo katika eneo la mashariki mwa Kongo.
Rais huyo wa Kongo ameyataja makubaliano hayo ya amani na Rwanda kuwa ya "kihistoria" na kusema ni "mabadiliko madhubuti" katika kumaliza mzozo huo, na kwamba ni ahadi ya amani kwa watu walioathiriwa na mzozo wa mashariki mwa Kongo kwa miongo kadhaa.