Tshisekedi kutohudhuria kikao cha AU juu ya vita vya DRC
14 Februari 2025Matangazo
Taarifa ya Ofisi ya Rais Tshisekedi imesema badala yake kiongozi huyo amekwenda nchini Ujerumani kushiriki kwenye Mkutano wa Usalama wa mjini Munich unaoanza leo hadi Jumamosi.
Kulingana na taarifa hiyo, Tshisekedi ataitumia fursa hiyo kuwasilisha ukweli kuhusu mzozo huo na kuomba ushirikiano zaidi wa jamii ya kimataifa katika kusaka suluhu na kuhitimisha shughuli za kijeshi kwenye eneo la Maziwa Makuu, na Jumamosi atahudhuria mkutano huo wa Umoja wa Afrika kwa njia ya mtandao.
Soma pia:Mzozo wa Kongo kutawala mkutano wa kilele wa AU
Waziri Mkuu wa Kongo, Judith Suminwa Tuluka lakini, atashiriki kikao cha Baraza la Amani na Usalama, kinachofanyika leo Ijumaa.