MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Tshisekedi awarai vijana kujiunga na jeshi kupambana na M23
30 Januari 2025Matangazo
Katika hotuba hotuba kwa taifa iliyorushwa kwa njia ya televisheni, Tshisekedi amewahimiza vijana kuingia jeshini akisema wao ndiyo wanabeba dhima ya ulinzi wa Kongo.
Kwenye hotuba hiyo Tshisekedi pia ameapa kuwakabilili kwa nguvu kubwa wapiganaji hao wanaoungwa mkono na taifa jirani la Rwanda
Amesema wanaandaa kampeni ya kujibu mapigo kwa ustadi na iliyoratibiwa vizuri dhidi ya magaidi hao (wa m23) na mfadhili wao (Rwanda).
Jumatano usiku wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walifanya mkutano kwa njia ya mtandao na kuitolea mwito Kongo kufanya mazungumzo na makundi ya waasi ikiwemo M23. Mkutano huo hata hivyo ulisusiwa na Rais Felix Tshisekedi.