Tshisekedi anapanga kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa
23 Februari 2025Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi anatarajiwa kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa, wakati akizidi kukabiliwa na shinikizo la ndani la namna anavyoshughulikia mashambulizi makubwa ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa nchi hiyo.M23 waelekea katika mji mwingine wa mashariki mwa DRC wa Butembo
Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya rais Tina Salama, Tshisekedi ataunda serikali ya umoja wa kitaifa na kufanya mabadiliko katika uongozi wa muungano huo, bila kutoa maelezo zaidi.
Hapo jana, Tshisekedi aliueleza mkutano wa muungano unaotawala wa kutoyumbishwa na mivutano ya ndani, akitoa wito wa kuungana zaidi kukabiliana na adui. Tangu kuanza kwa mwaka huu, Kongo imepoteza maeneo kadha ya majimbo ya Kivu Kusini na Kaskazini na kuchochea ukosoaji wa mkakati wa kijeshi wa serikali ya Tshisekedi.
Waasi wa M23 wanadhibiti miji ya Goma na Bukavu.