Tshisekedi akutana na mshauri wa Trump mjini Kinshasa
4 Aprili 2025Matangazo
Wawili hao walikutana mjini Kinshasa na walizungumzia kuhusu uwezekano wa kufikia makubaliano ya uchimbaji madini ya Kongo bila hata hivyo kuelezea ikiwa kutakuwepo ushirikiano wa kiusalama kati ya mataifa hayo mawili.
Boulos ni Mmarekani aliyezaliwa Lebanon na amemuoa mwanawe Trump, Tiffany na mbali na kuwa mshauri mkuu wa Afrika kwa Trump, pia ni mshauri mkuu kwa rais huyo wa Marekani katika masuala ya Mashariki ya Kati.