Tshisekedi abatilisha hukumu ya kifo dhidi ya wamarekani 3
2 Aprili 2025Matangazo
Msemaji wa rais wa Kongo Tina Salama, amesema hukumu hiyo ya kifo ilibatilishwa kwa amri ya rais na badala yake watuhumiwa hao sasa watatumikia kifungo cha maisha jela.
Watu 37 wahukumiwa kifo kwa jaribio la mapinduzi DRC
Hatu hiyo inakuja zaidi ya miezi sita baada ya mahakama ya kijeshi kuwahukumu watatu hao pamoja na washtakiwa wengine 30 kifo kufuatia mapinduziyaliotibuka yalioongozwa na kiongozi wa upinzani asiye maarufu Christian Malanga yaliolenga ikulu ya rais.
Kongo na Marekani zatia juhudi za ushirikiano
Msamaha huo unakuja wakati kukiwa na juhudi za mamlaka ya Kongo kutia saini makubaliano ya madini na Marekani kwa kubadilishana na msaada wa usalama katika mapambano yake na waasi mashariki mwa nchi hiyo.