Trump: Sijafurahishwa na ukaribu wa Urusi, India na China
5 Septemba 2025Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba, "Marekani imewapoteza India na Urusi kwa China yenye giza na kina kirefu, na kwamba anazitakia nchi hizo maisha marefu na yenye mafanikio ya pamoja."
Kauli ya kiongozi huyo wa Marekani ameitoa siku chache tu baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais wa China Xi Jinping kukutana wakati wa mkutano wa kilele wa shirika la ushirikiano la Shanghai SCO.
Katika mkutano huo uliofanyika mjini Tianjin, viongozi hao walisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina yao.
Putin na Xi pia walihimiza kuwepo kwa mpangilio mwengine wa kimataifa usioongozwa na Marekani na washirika wake wa Ulaya, wakitaka mfumo wa dunia wenye usawa na unaozingatia maslahi ya mataifa yote.