Trump na Putin kukutana muda mfupi ujao
15 Agosti 2025Rais Vladimir Putin wa Urusi anatarajiwa kuwasiliAlaska muda mfupi ujao kukutana na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, katika mkutano unaosubiriwa kwa hamu na ulimwengu. Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Ikulu ya Urusi ya Kremlin, Dmitry Peskov.
Mkutano kati ya viongozi hao wawili unatarajiwa kutoa mustakabali na maamuzi juu ya vita vya Urusi nchini Ukraine vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu.
Akielekea kwenye mkutano huo Rais Trumpamesema hatma ya kubadilishana maeneo ili kuvimaliza vita hivyo litakuwa juu ya Ukraine kuamua:
''Watajadilili wenyewe mabadilishano hayo lakini sina budi kuiruhusu Ukraine ifanye uamuzi huo. Na nadhani watafanya uamuzi sahihi. Lakini siko hapa kufanya mazungumzo kwa ajili ya Ukraine. Niko hapa ili kumleta Rais Putin kwenye meza ya mazungumzo, na nadhani tuna pande zote mbili hapa. Rais Putin alitaka kuichukua Ukraine yote na kama nisingekuwa rais kwa sasa angekuwa tayari ameshaichukua lakini kwa sasa hawezi kufanya hivyo'' Trump ameongeza.
Pamoja na matamshi hayo ya Trump bado Ukraine na washirika wake wa Ulaya wana hofu juu ya makubaliano yatakayofikiwa katika mkutano huo.