Trump na Putin kujadiliana kuhusu Ukraine wiki hii
17 Machi 2025Trump amesema mazungumzo tayari yanaendelea kuhusu kugawanya mali kadhaa kati ya pande hizo hasimu. Kulingana na Trump, ardhi na mitambo ya umeme ndiyo kiini cha mazungumzo ya kufikia amani kati ya Urusi na Ukraine.
"Na tutakuwa tunazungumza kuhusu ardhi, tutazungumza kuhusu mitambo ya umeme. Hilo, unajua ndiyo swali kubwa. Lakini nadhani tuna mengi ambayo tayari yamejadiliwa sana na pande zote mbili. Ukraine na Urusi. Tayari tunazungumza kuhusu hilo."
Soma pia:Zelensky: Urusi haionyeshi nia ya kuvimaliza vita
Jana, maafisa wa Marekani walielezea matumaini yao kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Ukraine na Urusi yanaweza kufikiwa katika wiki chache zijazo, baada ya Washington kupendekeza kusitishwa vita vya miaka mitatu, wakati wa mazungumzo ya Saudi Arabia, pendekezo ambalo Ukraine ililikubali huku Urusi ikiwa bado haijatoa jibu lolote kuhusu pendekezo hilo.