Trump: Mazungumzo ya kusitisha vita Ukraine kuleta tija
13 Aprili 2025Matangazo
Wajumbe wa Marekani na Urusi mapema wiki hii walifanya mkutano, na vyanzo vya karibu vinasema njia ya mafanikio ya kusitisha vita nchini Ukraine ni kuunga mkono mkakati wa kuipa Urusi umiliki wa maeneo manne ya mashariki mwa Ukraine ambayo ilijaribu kuyachukua kimabavu mnamo 2022.
Soma pia:Urusi na Uturuki zaijadili mizozo ya Ukraine, Mashariki ya Kati
Wakati hayo yakiendelea vikosi vya anga vya Ukraine vimedungua droni 43 kati ya 55 zilizovurumishwa na Urusi usiku wa kuamkia leo zikilenga maeneo ya kaskazini, kusini na katikati mwa Ukraine.
Jeshi la anga la Ukraine halikutoa taarifa zaidi juu ya uharibifu ama madhara ya kibinadamu kufuatia mashambulizi hayo ya anga ya Urusi.