Trump: Marekani kuitumia silaha zaidi Ukraine
8 Julai 2025Marekani imesema itatuma silaha ziadi nchini Ukraine, ikiwa ni wiki moja baada ya Ikulu ya White House kutangaza kusitisha baadhi ya shehena za silaha kuelekea mjini Kyiv wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, Rais Donald Trump amesema kwamba itabidi waipatie silaha Ukraine ili iweze kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi huku akiongeza kwamba hafurahishiwi na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Ukraine inakabiliwa na mashambulizi makubwa ya makombora na droni kutoka kwa Urusi katika vita vya miaka mitatu, na kusitishwa kwa utoaji wa silaha za Marekani kulififisha mapambano yake dhidi ya Urusi.
Alipoingia madarakani mwezi Januari Rais Trump aliweka shinikizo na jitihada kubwa za kuvimaliza vita hivyo ingawa mpaka sasa bado hazijazaa matunda.